MABINGWA wa kihistoria wa Kombe la Mapinudzi, Azam FC wameondolewa kwenye hatua ya nusu fainali na Yanga kwa kufungwa penalti 5-4 kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Amaan, visiwan Zanzibar.
Azam ikiwa imetwaa mataji hayo mara tano iliweka mzani sawa dakika ya 67 kupitia kwa Obrey Chirwa ambaye alisawazisha bao la kwanza kwa Yanga lililofungwa na Tuisila Kisinda dakika ya 51.
Ngoma ilikamilika dakika 90 bila kufungana ambapo kwa Azam FC kipa alikuwa ni Benedict Haule ambaye alichukua nafasi ya kipa aliyeanza Maseke Wilbol ambaye amepandishwa kutoka timu B.
Kwa Yanga alibaki langoni Faroukh Shikalo ambaye alikuwa shujaa wa mchezo wa leo licha ya kufungwa bao moja kwa uzembe wake baada ya kutoka kidogo langoni.
Kwa penalti tano za mwanzo ngoma ilikuwa ni 4-4 kwa timu zote mbili za Azam na Yanga ambapo penalti ya kwanza kupigwa ilikuwa ni Azam FC ambao walipiga kupitia Awesu Awesu penalti hiyo ikaokolewa.
Kwa upande wa Azam, Haule aliokoa penalti ya Michael Sarpong pekee na penalti ya sita kwa Azam ilipigwa na Daniel Amoah iliokolewa na Shikalo.
Kwa Yanga penalti ya ushindi ilifungwa na kiungo zawadi Mauya na kuifanya timu hiyo kutinga hatua ya fainali.
George Lwandamina amesema kuwa wameshindwa kutokana na kutokuwa na maandalizi mazuri.
Azam kidogo kidogo wanageuzwa kuwa wateja wa yanga
ReplyDelete