UONGOZI wa Klabu ya Simba umesema kuwa kabla ya mashindano ambayo wameyatambulisha ya SIMBA SUPER CUP ambayo yatashirikisha timu tatu hayajaanza watakuwa wameshamtambulisha kocha mpya.
Sven Vandenbroeck ambaye alikuwa Kocha Mkuu wa Simba alibwaga manyanga Januari 7 muda mfupi baada ya kuifikisha timu hiyo hatua ya makundi kwa ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya FC Platinum ya Zimbabwe.
Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez amesema timu tatu zitashiriki kwenye mashindano hayo ambazo ni Simba SC, TP Mazembe na Al Hilal ya Sudan. Mashindano yataanza Januari 27 hadi 31, 2021
Barbara amesema:"Kabla ya mashindano kuanza tutakuwa tumeshamtangaza kocha mpya hivyo kesho mashabiki watamjua kocha mpya wa Simba wasiwe na mashaka.
"Kikubwa ni kwamba tupo imara hatuna mashaka yoyote mashabiki wasiwe na mashaka kila kitu kitakwenda sawa," .
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa malengo makubwa ya kumleta kocha huyo yapo wazi ni kwenye kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara pamoja na kufanya vizuri kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.
Hayo yote kwa uwezo wa Mwenyezimungu tunaemtegemea yatakuwa
ReplyDelete