January 27, 2021


UONGOZI wa Mtibwa Sugar umeweka wazi kwamba utapambana kufanya vizuri ndani ya Ligi Kuu Bara kwenye mzunguko wa pili.

Mtibwa Sugar ipo chini ya Kocha Mkuu, Hitimana Thiery ambaye ameibuka ndani ya kikosi hicho baada ya kupigwa chini na kikosi cha Namungo FC

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobisa Kifaru amesema kuwa watafanya kazi kwa uzuri ili kupata matokeo mazuri.

"Kwa sasa maumivu ya kupoteza Kombe la Mapinduzi, tumeweka kando kabisa akili yetu sasa ni ndani ya Ligi Kuu Bara.

"Tunajua mzunguko wa pili utakuwa mgumu na kila timu inasaka matokeo hivyo nasi tutapambana kufanya vizuri," .

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic