January 27, 2021


 KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes kimeibuka na ushindi wa mabao 4-1  dhidi ya Al Hilal kwenye mchezo wa Simba Super Cup.
 
Mchezo huo umechezwa leo Januari 27,Uwanja wa Mkapa na ulishuhudiwa na mashabiki wengi ikiwa ni pamoja na wale waliokuwa wamevaa jezi ya Klabu ya Yanga huku wakionekana kuwa na furaha muda wote.

Ikiwa ni mchezo wa kwanza kwa Gomes ambaye amerithi mikoba ya Sven Vandenbroeck ambaye ametimkia Morocco katika Klabu ya FAR Rabat alishuhudia uwezo wa nyota wake ikiwa ni pamoja na Rarry Bwalya aliyeanza kupachika bao la kwanza dakika ya 39.

Bao hilo lilisawazishwa na Salim Mohamed wa Al Hilal baada ya mabeki wa Simba kufanya uzembe huku Beno Kakolanya akishindwa kuokoa mchomo wa kichwa dakika ya 45.

Kipindi cha pili Perfect Chikwende alipachika bao la pili dakika ya 72 baada ya kipa wa Al Hilal kutema shuti lililopigwa na Bernard Morrison ambaye aliingia kipindi cha pili.

Morrison aliweza kufunga mabao mawili ambapo bao la tatu likiwa ni la pili kwake alifunga dakika ya 86 na lile la pili kwake likiwa la nne kwa Simba alifunga dakika ya 89.

Kocha Gomes amesema kuwa wachezaji wake walipambana kusaka ushindi jambo ambalo limewafanya waweze kuibuka na ushindi huo.

"Wachezaji wamepambana kusaka ushindi na wamefanikiwa hivyo naona kwamba wanastahili pongezi kwa kile ambacho wamekifanya," .


18 COMMENTS:

  1. KWELI YANGA MNAJUA KUTENGENEZA PICHA FAKE DAH AMAKWELI NIMEAMIN NYIE NDIO WANANCHI WA NCHI HII. YANI MNACHEZA MNAVYOTAKA NYINYI MNAFANYA MNALOONA LINAFAA KWENU, ILA UPO WAKATI MALIPO YATAKUJA. MNA MDHALILISHA MORISON KWANINI UNA EDIT PICHA KUTENGENEZA SAIKOLOJIKO IMPAKTI ITAKAYOLETA MADHARA KWA JAMII HUSIKA.

    ReplyDelete
  2. Ukiambiwa kuna watu wajinga basi ndio design hii. Kwa kitendo hiki mtu akipelekwa mahakamani hachomoki.

    ReplyDelete
    Replies
    1. hiyo ni picha halisi wakati bm3 akishangilia goli kwenye mechi leo ,ni ishara ya kuwaonyesha wale waliodai ana ... amefunga goli mbili so anawajibu waliosambaza habari za ugonjwa huo

      Delete
  3. Ila haiwasaidii chochote maana wenye akili wameshajua kuwa tunadeal na watu wajinga. Mpira umewashinda wamekalia kuunda ujinga

    ReplyDelete
  4. Al Hilal bingwa wa Sudan hakuweza kumziwiya Kingi wa misitu na juu ya ushangiliaji wa kikundi kidogo cha yanga kilichofika pale kwa kmtakia mabaya Mnyama, lakini Mungu hakuwa pamoja nao wakamuona Mnyama hihivi wakimtesa bingwa wa Sudan. Mtego ukimnasa kanga, hatusemi asante kanga lakini tunasema asante Mtego kwahivo nasi twasema asante kocha aliyekiongoza vyema kikosi katika siku yake ya kwanza na kikosi kilichofanya na kuyatimiza ambapo wachezaji waliyatimiza kwa kutumia mstsari na kalamu. Kiwango kilikuwa cha kupigia mfano. We are looking forward for the best

    ReplyDelete
  5. Dah hawa jamaa wanakosea sana,Ila mungu anawaona na atawahukumu kwa hili,YANGA badilikeni jaman.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwani Yanga ndo wamiliki wa blog hii?

      Delete
  6. Kama hio picha ni ya kuedit ( na inaonekana kweli ni ya kuedit) kwa nini mmiliki wa blog hii asipelekwe mbele ya sheria?

    ReplyDelete
  7. Al hilal Al obeid msimu uliopita amemaliza akiwa nafasi ya pili,hizi ni salam kwa jirani Unaekereketwa na roho. Mungu akuweke Uje ushuhudie kichapo utakachopewa na mnyama pindi mtakapokutana.

    ReplyDelete
    Replies
    1. List hii ikutane na Ruvu Shooting tuu ndio mtaelewa

      Delete
  8. Nilishasema hii blog ipo siku itafika watu wataacha kusoma habar zao, walichokifanya ni ujinga mtupu na wanastahili kufungiwa hawa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Blog imefanya ujinga upi, wewe ndio mjinga ambae una toa maoni na kitu usichokijua.

      Delete
  9. Hawana weledi katika kazi yao, wapo kishabiki zaidi... UTOPOLO tu umewajaa

    ReplyDelete
  10. Wivu na roho mbaya vimewajaa ndo maana wanaroga wachezaji

    ReplyDelete
  11. Wengi mnaokoment hamkutazama mpira,fahamu kwamba MORISON alichukua mpira akauweka huko chini yeye mwenyewe, Hakuna editing hapo kama umetazama mpira utaniunga mkono.msipende kumvalisha YANGA lawama kwa kila jambo baya na la hovyo jaman.

    ReplyDelete
  12. Tatizo la waTz mtu anaweza kubisha kitu asichojua, Sasa hata mpira hajaangalia anasema picha wameEdit, kuishi na jamii ya aina hii ni hatari sana

    ReplyDelete
  13. Yaan watu Wana comment kitu wasichokijua kabisa, eti picha editing wakati hata mpira hawakuangalia.

    ReplyDelete
  14. Kwani watu wanabishana nn apa, morrison kaweka mpira mwenyewe kwenye pumbu, je anaashiria nn? Badala ya kutafakar kwann kafanya hivyo mnalalama et picha ya editing! Kwan si kaweka mwenyewe

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic