KIKOSI cha Namungo FC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Hemed Morroco leo Januari 3 kimeanza safari kuelekea Sudani.
Kikosi hicho kikiwa kimeongozana na viongozi ikiwa ni pamoja na Mwenyekiti, Hassan Zidadu kitatua Addis Ababa kisha kitaunganisha kuelekea Khartoum Sudani.
Namungo inakwenda kwa ajili ya mchezo wa marudio wa Kombe la Shirikisho dhidi ya El Hilal Obeid unaotarajiwa kuchezwa Januari 6.
Kazi kubwa ni kulinda na kusaka ushindi ili kusonga mbele kwa kuwa mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, Desemba 23,2020 Namungo ilishinda mabao 2-0.
Morroco amesema:"Tunakwenda kupambana kwenye mchezo huo na tunaamini kwamba utakuwa mchezo mgumu na wenye ushindani mkubwa nasi tutafanya vizuri.
"Mashabiki watuombee dua ili tufanye vizuri hakuna mashaka katika makosa ambayo tuliyafanya wakati uliopita kwenye mchezo wetu, tupo tayari kufanya vizuri," .
Kila la kheri wawakilishi wetu
ReplyDeleteMwenyezi Mungu awe nanyi ktk safar pia ktk kupambania taifa
ReplyDeleteSio El Hilal obeid ni Al Hilal El Obeid. Waandishi makanjanja.
ReplyDeleteMaombi yetu yapo kwenu wawakilishi wetu.
ReplyDelete