January 27, 2021

 


OPPAH Clement mshambuliaji wa kikosi cha Simba Queens amekuwa ni mchezaji wa kwanza kufunga mabao saba ndani ya Ligi ya Wanawake msimu wa 2020/21.

Mshambuliaji huyo ni miongoni mwa washambuliaji wazawa wanaofanya vizuri ndani ya ardhi ya Bongo kwa sasa.

Alitupia mabao hayo wakati timu yake ya Simba Queens ikiibuka na ushindi wa mabao 11-1 dhidi ya TSC Queens, mchezo uliochezwa Uwanja wa Mo Simba Arena. 

Ilikuwa  Januari 25  wakati mabingwa hao watetezi wa taji la Ligi ya Wanawake Tanzania wakisepa na pointi tatu muhimu.

Matokeo hayo yanaifanya Simba Queens kuwa nafasi ya pili na pointi zake ni 29 baada ya kucheza mechi 11 huku kinara akiwa ni Yanga Princess mwenye pointi 31.

Jumla mshambuliaji huyo mzawa anafikisha jumla ya mabao 20 kibindoni.

Nyota huyo amesema:"Malengo makubwa ni kuona timu inapata matokeo, ushindi ni furaha kwetu pamoja na mashabiki tunahitaji sapoti," .

4 COMMENTS:

  1. siku hizi kila siku lazima muandike kuhusu ligi ya wanawake...halafu ambapo hata vinara wa ligi hawausiki kabisa lazima mkumbushie "ambapo vinara wa ligi hiyo ni.." Imekuwa kama Yanga hapo nyuma ilivyokuwa ikilichukulia kombe la mapinduzi..huwa hawapeleki kikosi cha kwanza...etk wana mipango na ubingwa ligi kuu, sportpesa na FA cup.Mwaka huj walipogundua Simba imepumzisha baada ya kufuzu na wengine wengi wako Stars...basi kombe la Mapinduzi limegeuka lulu.Sisi tunawacheki tu
    uandishi wenu haufai!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni wewe ndiyo uso ajili wako haufai, nwatakukera sanaaaa

      Delete
    2. Ni wewe ndiye usomaji wako haufai. Watakukera sanaaaa!

      Delete
  2. Double hatrick + 1 Hahahaa Hongera sana dada

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic