January 27, 2021

 


KIUNGO mkabaji wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Baraka Majogoro, amefunguka kuwa wamejipanga kupambana kwa nguvu kubwa kuhakikisha wanawafunga Guinea na kutinga hatua ya robo ya kombe la Chan.

 

Majogoro ameongeza kuwa akili yao kwa sasa wameielekeza katika mchezo huo wa mwisho wa Kundi D.


Stars inayonolewa na Kocha Mkuu, Etienne Ndayiragije ilishinda bao 1-0 dhidi ya Namibia juzi,ipo nafasi ya tatu katika msimamo wa Kundi D ikiwa na pointi tatu ikizidiwa pointi moja na Zambia na Guinea ambao ni vinara.

 

Stars wanaofundishwa na kocha Ndayiragije, wamebakisha mechi ya mwisho dhidi ya Guinea ambayo itaamua timu mbili ambazo zitaenda hatua ya robo fainali.


 Mechi hiyo inachezwa leo Jumatatno Januari 27.

Majogoro ambaye anaichezea Mtibwa Sugar amesema, kuwa wana imani wakijitoa na kupambana wana uhakika wa kusonga katika hatua ya robo fainali.

 

“Tupo tayari kwa ajili ya ushindani na tunatambua kwamba utakuwa mchezo mgumu ila hawataweza kututoa kirahisi ndani ya dakika 90.


“Lakini siamini kama wataweza kututoa, kivyovyote vile tutapita kwenda robo fainali kwani tutapambana vya kutosha uwanjani,” alimaliza Majogoro.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic