NYOTA tisa wa kikosi cha kwanza ndani ya Yanga wanatajiwa kukosa michuano ya Kombe la Mapinduzi ambalo linatarajiwa kuanza kutimua vumbi kesho, Januari 5 .
Bingwa mtetezi wa taji hilo la heshima litakalofanyika visiwani Zanzibar ni Mtibwa Sugar ambaye atafungua pazi hilo kesho, Januari 5 kwa kuanza kumenyana na Chipukizi saa 10:15 jioni.
Mchezo wa kwanza kwa Yanga ambayo itasepa leo ni dhidi ya Jamhuri utakaochezwa saa 8:15 Uwanja wa Amaan.
Nyota hao ni Yassin Mustapha, Bakari Mwamnyeto, Farid Mussa, Feisal Salum, Ditram Nchimbi na Deus Kaseke ambao wapo kwenye kambi ya timu ya Taifa ya Tanzania inayojiandaa na michuano ya Chan 2021.
Balama Mapinduzi yeye ni mgonjwa na kiungo Carlos Carlinhos huku Yacouba Songne akiwa amepewa mapumziko ya wiki moja kutibu majeraha yake ya mbavu.
0 COMMENTS:
Post a Comment