OFISA Habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara, amesema kuwa kiungo mzawa Jonas Mkude hajafukuzwa ndani ya kikosi hicho bali suala lake lipo kwenye kamati ya nidhamu.
Desemba 28, taarifa rasmi kutoka Simba ilieleza kuwa kiungo huyo ambaye ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck amesimamishwa ndani ya kikosi hicho kutokana na utovu wa nidhamu.
Tayari amekosa mechi mbili ambapo ya kwanza ilikuwa ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Majimaji na ule wa pili wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ihefu FC zote zilichezwa Uwanja wa Mkapa.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam,leo Januari 4 Manara amesema suala la mchezaji Jonas Mkude bado lipo kwenye kamati ya nidhamu ya Simba.
"Kuhusu Jonas Mkude ijulikane tu kuwa mpaka sasa ni sehemu ya Simba hajafukuzwa kazi, amepitia changamoto kama mfanyakazi mwingine kokote.
“Mkude ni mchezaji wa Simba. Jambo lake lipo kamati ya maadili. Mkude hajafukuzwa Simba. Bila shaka yoyote baada ya kamati atarejea klabuni. Huyu ndiye mchezaji mwandamizi ndani ya Simba kwa miaka 10.” amesema.
Simba ina kibarua cha kumenyana na FC Platinum Januari 6, Uwanja wa Mkapa ikiwa ni mchezo wa marudio baada ya ule wa kwanza kupoteza kwa kufungwa bao 1-0.
Ili kutinga hatua ya makundi ina kazi ya kusaka ushindi wa mabao zaidi ya mawili na kulinda lango lao lisiguswe na wapinzani.
Aende tuu kama hataki kubadilika
ReplyDeleteMh! Anavimba kichwa na kufanya atakacho kwa kauli kama hizi eti: "mchezaji mwandamizi ndani ya Simba kwa miaka 10". Ni kweli, kama hawezi kubadilika au kaichoka Simba aondoke haraka. Iwe ni mpira au kazi nyingine yoyote, nidhamu ni kitu cha msingi sana.
ReplyDeleteKwa kauli kama hiyo ya manara unategemea atabadilika vipi.....nini maana ya kamati ya maadili?.unapoitwa kwenye kamati yoyote ya maadili maana yake unaweza usikutwe na kosa maisha yakaendelea,au ukakutwa na kosa ukapewa adhabu au kufukuzwa kazi....manara anapotuambia kuwa kamati ya maadili ikimaliza kazi yake mkude ataendelea na maisha ndani ya simba kama kawaida anataka kutuambia nini?,kwamba ana uhakika kuwa hana kesi ya kujibu au hata kama atakutwa na kesi hawezi kuadhibiwa!!!!!???
DeleteHawa kina Manara ndio wanampa kichwa Mkude hata angechezea miaka 20 kama hawezi kuheshi jezi ya Simba aende kulikuwa na viungo bora kama kina Lenny, Njohole au Marshal lakini hawakuwa na nidhamu mbovu kama ya Mkude
ReplyDeleteYou are saying something very important!
DeleteMsiwe na wasiwasi wadau, mbona hata ulaya watu wanawekwa kando tu? YAHYA TOURE ALIWEKWA KANDO NA PEP
DeleteUpo sahihi kbs Rodrick.
DeleteMimi upande wangu nadhani Yale ya mtu kujifanya anajua kila kitu ndiyo madhara yake,kukutana au kuitwa na Kamati ya maadili siyo kusema kuhukumiwa kifo au unakosa lisilo sameheka .Naona wanahaki ya kumlinda mtu na kumpa haki cse walishakosea hapo awali waliyosoma amesimamishwa kwa utovu wa nidhamu Lakini upi? ,kwangu Mimi hizi ni tuhuma tu mjue .Kwa kuwa bado ni Mchezaji wao wanahaki kutoa taarifa ya kumlinda .
ReplyDeleteHapo kuna mchezo wa Psychology unachezwa, usije shangaa ukamuona kwenye mchezo wa Platinum Fc
ReplyDelete