January 9, 2021


 UPO uwezekano mkubwa wa mshambuliaji wa kimataifa wa Yanga raia Mghana Michael Sarpong kuondoka kati ya mwanzoni au mwisho mwa msimu huu baada ya kupata dili la kucheza nje ya nchi.

 

Mghana huyo hivi sasa ameonekana kutokuwa na mchango mkubwa katika kikosi cha Mrundi Cedric Kaze mwenye mabao manne pekee katika msimu huu wa Ligi Kuu Bara.

 

Awali, Yanga ilikuwa ina matarajio makubwa na Mghana huyo kabla ya kujiunga na timu hiyo katika msimu huu akitokea Rayon Sports ya nchini Rwanda.


Habari zinaeleza kuwa mshambuliaji huyo yeye mwenyewe ndiye anataka kuondoka baada ya kupata ofa kwenye moja ya klabu ya nje ya nchi.

 

Mtoa taarifa huyo amesema kuwa mshambuliaji huyo tayari ameutaarifu uongozi wa timu hiyo, lakini bado hajapatiwa majibu juu ya suala hilo.Aliongeza kuwa kama uongozi utakubaliana na mshambuliaji huyo, basi upo uwezekano mkubwa wa kuondoka katikati ya msimu au mwishoni baada ya ligi kumalizika.


“Sarpong hivi karibuni aliutaarifu uongozi juu ya yeye kupata ofa nzuri ya kwenda kucheza soka nje ya nchi baada ya kupata ofa nzuri.

 

“Lakini uongozi bado haujampa majibu juu ya hilo, bado mazungumzo yanaendelea kama yakienda vizuri, basi ataondoka Yanga na kwenda huko anapotaka kwenda,” alisema mtoa taarifa huyo.

 

Alipotafutwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga Injinia, Hersi Said kuzungumzia hilo simu yake ya mkononi iliiita bila ya mafanikio ya kupokelewa.


Ndani ya Yanga ambayo inaongoza Ligi Kuu Bara kwa sasa ikiwa nafasi ya kwanza na pointi 44 ikiwa imetupia mabao 29 ametupia mabao manne.


Chanzo:Championi

4 COMMENTS:

  1. Usije ukashangaa kuwa huenda alisaini miezi sita. Timu zeti ubabaishaji mwingi mno kwenye usajili

    ReplyDelete
    Replies
    1. unachangia hata maji ya kunywa wewe tuliza mshono huo ujifunze kuandika pussyfc

      Delete
  2. Hayo wasema wewe. Umeambiwa mchezaji ameomba kuondoka baada ya kupata offer nzuri sehem nyingine, wewe unasema inawezekana alisaini mkataba wa miezi sita. hivi nyie watu lini mtaacha kupiga lamli? manake hyo ni sawa na kupiga lamli.

    ReplyDelete
  3. Sio lamli ni ramli. Zingatia kiswahili fasaha

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic