January 9, 2021

 


WACHEZAJI wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars leo Januari 9 wamefanyiwa vipimo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete,(JKCI).

Hii ni sehemu ya maandalizi kuelekea kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya DR Congo pamoja na maandalizi ya CHAN yatakayofanyika nchini Cameroon.

Stars imekuwa ikipewa sapoti kutoka Serikalini ambapo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bushungwa na Naibu wake Abdallah Ulega wamekuwa wakizungumza na wachezaji pamoja na kutembelea mazoezi ambayo yanafanyika Uwanja wa Mkapa.

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu, Tanzania, (TFF), Wallace Karia amesema kuwa wanashukuru kwa sapoti wanayopata kutoka Serikalini.


"Kwa namna ambavyo mmekuwa bega kwa bega nasi ni furaha na tunasema asante kwa kuwa ni faraja kwa wachezaji pamoja na sisi viongozi hivyo tunatambua kazi yetu ni kuweza kurejesha furaha kwa Watanzania kwa kupata matokeo mazuri ndani ya uwanja," .


Mchezo wa kirafiki unatarajiwa kuchezwa Januari 12, Uwanja wa Mkapa na utakuwa rasmi kumuaga nyota Agrey Morris beki mkongwe anayetumika ndani ya Klabu ya Azam FC.

Beki huyo ametangaza kujiweka kando kwenye masuala ya kuitumikia timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic