January 14, 2021




 KIKOSI cha Yanga kimeibuka na ubingwa wa Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa penalti 4-3 dhidi ya Simba baada ya dakika 90 kukamilika kwa sare ya kufungana.

Nyota wa mchezo huo ni Farouk Shikalo ambaye aliokoa penalti moja ya Joash Onyango na Meddie Kagere kugongengesha mwamba penalti yake moja.

Saido Ntibanzokiza ambaye alikuwa msumbufu ndani ya dakika zote 90 amesema kuwa wachezaji wenzake walimuomba awape sapoti naye akasema  kwamba hana tatizo atafanya kazi.

Alifunga penalti ya mwisho iliyomshinda mlinda mlango Beno Kakolanya ambaye hakuwa na namna baada ya kuoka hatari tano ndani ya dakika 90.

"Ilikuwa sijapangwa kucheza ila wachezaji waliomba nicheze nami nikasema kwamba nitacheza kwa kuwa mchezo ni kazi yangu na nimefanya hivyo ninafurahi.

"Mashabiki wangu na mashabiki wa Yanga ni wakati wetu wa kuendelea kupena sapoti," .

Huu unakuwa ni ubingwa wa pili kwa Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze huku Simba ikibakiwa na mataji yake matatu ndani ya kabati lao.

14 COMMENTS:

  1. Sio siku nyingi simba watamkumbuka Sven.Nilitaka kusikia wale wanaolalamika kuwa kagere hakupangwa? Kingine kama kagere ameshindwa kueka angalau goli la kuotea kambani mbele ya Abdala shaibu sijui huko kimataifa itakuaje? Kagere ni fowadi mzuri ila hajawi kuisadia simba kunako mechi ya ushindani yaani hajawahi kuwa mchezaji wa kuamua mechi kwenye mchezo kuipeleka simba sehemu fulani,chama keshafanya hivyo mara kadhaa takwimu zipo wazi.Fuatilia michezo ya kimataifa ya simba kagere ana magoli mangapi? Watu wanaposema ili simba kufanya vizuri klabu bingwa Africa lazima wasajili mshambuliaji mwenye uwezo wa ziada kuliko akina kagere sio shinikizo bali ni uhalisia wa mambo.

    ReplyDelete
  2. Kagere alifunga dhidi ya Al Ahly. Alifunga dhidi ya Nkana, alifunga dhidi ya Mbabane.
    Amechukua kiatu cha ufungaji bora mara mbili mfululizo.
    Wachezaji wote mashuhuri wanakosa penalti.
    Kagere sio tofauti na washambuliaji wengine waliokosa penalti.

    ReplyDelete
  3. Kocha wa Yanga kama anaisaidia simba vile kwani baada ya mchezo wa fainali ya mapinduzi cup alipohojiwa na mwanahabari kuwa aliwaonaje wapinzani wake yaani simba? Kaze hakumumunya maneno alisema simba bila ya chama na Miquisone ni wa kawaida mno.Ila nilitamani kumsikia kaze ukisema simba bila ya fowadi wao fulani huwa wa kawaida. Kwa maana hiyo pia kaze anajua kabisa siku akicheza na simba akifanikiwa kumkamata chama hukuna goli kwa simba.

    ReplyDelete
  4. Penati Ni mchezo wa bahati, hivyo bahati Jana ilikuwa kwa utopolo Sasa utopolo acheni kelele

    ReplyDelete
    Replies
    1. Si kweli. Ata short on target SIFULI. Semeni tu Paka alibaki Dar

      Delete
  5. Simba bila chama bila miquisone ni wa kawaida lkn dk 90 bila bila

    ReplyDelete
  6. VIMBURU kimya!!!!!

    ReplyDelete
  7. nguruwe fc hoiiiii, inaonekana paka wenu alibaki bara

    ReplyDelete
  8. Ujinga sio tusi ni mjinga asiyejua yanga babalao

    ReplyDelete
  9. Yanga kama kachukua klabu bingwa Africa vile.khaa.��

    ReplyDelete
  10. Mimi nadhani hata Kama tumeshinda mtu aliyekosa game plan ni Matola ,anashindwa kutofautisha Yanga na Namungo,ningekuelewa yeye ningeanza na Kagere na Mugalu huyo Miraji Hana uwezo wa kucheza mechi ya Yanga hii na zaidi Ajibu angekuwa better option kuanza nafasi ya Kahata.

    ReplyDelete
  11. Hiyo ndio maana halisi ya utopolo Simba kaingia makundi klabu bingwa afrika shangwe lilikuwepo lkn kwa shangwe la Jana like la kuchukua mapinduzi au kuifunga Simba Tena kwa penalti inadhiirisha ukubwa was Simba kwenye soka la Tanzania na muda si mrefu tutakuwa wababe afrika mzima,najua tumbili fc ways comment hapa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic