OFISA Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Azam, Abdulkarim Amin ‘Popat’ amesema kuwa wanahitaji kuongeza wachezaji ndani ya kikosi hicho huku akigusia suala la kiungo Perfect Chikwende ambaye amekuwa akitajwa kuibukia ndani ya kikosi hicho.
Perfect jina lake limekuwa likitajwa kuingia kwenye rada za Azam FC baada ya kuonyesha uwezo kwenye mechi za kimataifa ndani ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Alimtungua kipa namba moja wa Simba, Aishi Manula kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliochezwa Uwanja wa Taifa wa Zimbabwe.
Jitihada za Chikwende zilikutana na kisiki Uwanja wa Mkapa kwenye mchezo wa marudio ambapo alishuhudia timu yake ikipoteza kwa kufungwa mabao 4-0 na kufungashiwa virago Ligi ya Mabingwa Afrika na kwa sasa wapo ndani ya Kombe la Shirikisho.
Popat amesema: “Tunahitaji kufanya usajili kwenye kikosi chetu ili kuwa imara na sehemu ambayo tunahitaji ni kwenye kiungo pamoja na mshambuliaji.
"Bado tunapambana kupata kiungo kwa kuwa tayari tuna mshambuliaji mmoja ambaye tumemalizana naye hivyo ni suala la kusubiri na kuona," .
Azam FC imemalizana na Mpiana Monzinzi ambaye kwenye mchezo wake wa kwanza wa Kombe la Mapinduzi dhidi ya Mlandege wakati Azam FC ikishinda bao 1-0.
Azam ipo chini ya Kocha Mkuu, George Lwandamina ambaye kwa sasa kikosi chake kipo visiwani Zanzibar kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Mapinduzi.
Leo itafunga pazia kwa kucheza dhidi ya Malindi FC ikishinda itatinga hatua ya nusu fainali.
0 COMMENTS:
Post a Comment