January 6, 2021


KOCHA Mkuu wa FC Platinum ya Zimbabwe, Norman Mapeza ameweka wazi mbinu atakayotumia kuimaliza Simba kwenye mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa ni kuwashambulia wapinzani wake mwanzo mwisho ili kuwapa presha ya kufanya makosa.

 

Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck leo Januari 6 itashuka Uwanja wa Mkapa ikiwa na kibarua cha kupindua matokeo kwa kuwa mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Taifa wa Zimbabwe, ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 lililopachikwa na Perfect Chikwende.

 

Akizungumza na Saleh Jembe, Mapeza amesema kuwa mpango mkubwa ni kumaliza mchezo ndani ya dakika za mwanzo kwa kushambulia lango la mpinzani.

 

“Ulimwengu wa mpira umebadilika, nimewaambia wachezaji wangu hakuna kujilinda ni lazima tushambulie bila kukaa nyuma, hilo litatupa nguvu ya kupata ushindi mapema. Tunawaheshimu wapinzani wetu ila hatuwaogopi.

"Tumecheza nao mchezo wa kwanza pia nilipata nafasi ya kuona namna ambavyo wanacheza, ikiwa UD Songo waliweza kupata matokeo je sisi ni nani tusipate matokeo?

Kocha wa Simba, Sven amesema kuwa anatambua walikosea mchezo wao uliopita ila wamefanya kazi ya kurekebisha makosa yao ili wapate matokeo mazuri.

 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic