FAROUK Shikalo kipa wa Klabu ya Yanga amesema kuwa bado wana nafasi ya kufanya vizuri kwenye mashindano ya Kombe la Mapinduzi licha ya kukosa kupata ushindi kwenye mchezo wa ufunguzi uliochezwa Uwanja wa Amaan, jana Januari 5.
Yanga ilikamilisha dakika 90 bila kupata bao mbele ya Jamhuri ya visiwani Zanzibar mchezo ambao ulikuwa na ufundi mwingi kwa timu zote kucheza mpira wa pasi na kushambuliana kwa zamu.
Shikalo amesema kuwa wachezaji walifanya kazi yao ndani ya uwanja kwa kujituma ila bahati haikuwa upande wao kwa kuwa wapinzani wao waliweza kuzuia makosa yao.
"Wapinzani waliweza kuzuia makosa yao ambayo tulipaswa tuyatumie kuwa mabao, ila kwa kuwa ni mwanzo bado tuna nafasi ya kufanya vizuri.
"Huu ni mwanza na siku zote kadri unavyoanza ndivyo utakavyomaliza kwangu mimi pamoja na timu bado nina amini tuna kazi ya kufanya kwa ajili ya mechi zijazo," amesema.
Ikiwa kundi A ipo pamoja na timu ya Namungo ambayo itarejea leo kutoka Sudani baada ya kumaliza jana mchezo wa kimataifa dhidi ya Al El Hilal Obeid na kulazimisha sare ya kufungana mabao 3-3, Uwanja wa Al Hilal.
Ushindi huo unaifanya timu hiyo isonge mbele hatua inayofuata kwa kuwaondoa wapinzani wao kwa ushindi wa jumla ya mabao 5-3 kwa kuwa mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Azam Complex ilishinda mabao 2-0.







0 COMMENTS:
Post a Comment