UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa kazi ya kusaka ubingwa kwa msimu wa 2020/21 ipo palepale licha ya kumaliza kwa kupata sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Tanzania Prisons kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Nelson Mandela.
Ikiwa imecheza jumla ya mechi 18 imeshinda mechi 13 na ina sare tano na pointi zake ni 44 kibindoni ikiwa nafasi ya kwanza kwenye msimamo.
Akizungumza na Saleh Jembe, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa malengo makubwa ya timu hiyo ya kutwaa ubingwa hayajawekwa kando.
“Nia yetu ipo wazi kwa msimu huu ni kuona kwamba tunanyanyua mikono kunyayua ubingwa wa Ligi Kuu Bara hilo lipo wazi hivyo mashabiki wazidi kutupa sapoti.
“Ushindani ni mkubwa hilo tunalitambua ila nasi pia tunapambana kupata matokeo chanya ndani ya uwanja,mashabiki watupe sapoti kwani kikosi tulicho nacho ni maalumu kwa ajili ya kutupatia ubingwa,” amesema.
Yanga inafuatiwa na Simba ambao ni mabingwa watetezi wakiwa nafasi ya pili na pointi zao ni 35 baada ya kucheza mechi 15 ndani ya ligi.
Hesabuni usiku na mchana lakini ubingwa bado ni ndoto
ReplyDelete