NAHODHA wa kikosi cha Arsenal, Pierre Emerick Aubameyang amewashukuru wachezaji wenzake pamoja na benchi la ufundi kwa sapoti ambayo wamekuwa wakimpa pamoja na kurejea kwake kikosi cha kwanza baada ya kurudi kutoka kumuuguza mamaye ambaye anaumwa.
Nahodha huyo wa Arsenal ambaye ni raia wa Gabon jana Februari 14 alianza kwa mara ya kwanza kikosi cha kwanza tangu Januari 19 na katika mechi hiyo alifunga hat trick mbele ya Leeds United.
Akiwa Uwanja wa Emirates, kwenye ushindi wa mabao 4-2, Aubameyang alitupia mabao hayo dakika ya 13,41 kwa penalti na dakika ya 47 na lingine moja lilitupiwa na Hector Bellerin dakika ya 45.
Kwa upande wa Leeds watupiaji walikuwa ni Pascal Strujik dakika ya 58 na Helder Costa dakika ya 69. Matokeo hayo yanaifanya Arsenal kufikisha pointi 34 ikiwa nafasi ya 10 na Leeds ipo nafasi ya 11 na pointi zao ni 32.
Auba amesema:"Ninawashukuru wachezaji wenzagu, benchi la ufundi kwa sapoti ambayo wamekuwa wakinipa kwenye matatizo ambayo nimekuwa nikipitia.
"Nimefurahi kwa kufunga nina amini kwamba familia yangu itapata mpira wa kuchezea baada ya zawadi hii ambayo nimepata,".
0 COMMENTS:
Post a Comment