February 15, 2021


 MICHAEL Sarpong, mshambuliaji wa kikosi cha Yanga amesema kuwa ana matumaini ya kurejea kwenye ubora wake na kufunga mabao kwenye mzunguko wa pili tofauti na mzunguko wa kwanza mambo yalivyokuwa.

Sarpong mzunguko wa kwanza alimaliza akiwa ametupia mabao manne sawa na Yacouba Songne na Deus Kaseke ambaye yeye amejiengua kwenye eneo hilo kwa kuwa ametupia bao lake la tano mbele ya Mbeya City.

Sarpong kwenye mchezo wake wa kwanza wa mzunguko wa kwanza alifunga bao mbele ya Tanzania Prisons Uwanja wa Mkapa kwenye sare ya kufungana bao 1-1 ila safari hii kwenye mzunguko wa pili alikwama kutupia mbele ya Mbeya City, Uwanja wa Sokoine.

Nyota huyo amesema:"Ninatambua kwamba mashabiki pamoja na wachezaji wenzagu wanapenda kuona tukishangilia ila nina amini kwamba itakuwa hivyo ni suala la muda tu.

"Mimi ninapenda kufunga kwa kuwa mpira ni kazi yangu hivyo wakati huu nina amini kwamba nitafanya vizuri hivyo muhimu kuwa na subira,".

Yanga ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 45 baada ya kucheza jumla ya mechi 19, imefunga jumla ya mabao 30.

Ina kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Kagera Sugar, Februari 17, Uwanja wa Mkapa.

3 COMMENTS:

  1. Yaleyale. ya Zahera. Kutokana na droo na Mbeya City insyokamata mkia, Kocha Kaze keshaanza kulalamika waamuzi, jee na ile African Sport vilevile waamuzi? . Huenda madeni sugu ya Tambwe yasiyolipwa yameanza kuwatisha nyota na kupoteza morali

    ReplyDelete
    Replies
    1. YAANI KAULI YAKO INAWEZA KUFANYIWA UTAFITI YANGA. MAANA KUNA KILA DALILI KWAMBA PUMZI IMEKATA KWA GSM. IKIWA TIMU KAMA MBEYA CITY MNASHINDWA KUIFUNGA ILI HALI WAMETIMIA UNADHANI KUNA NINI? HIVI ZILE MILIONI 300 ZA GSM KAMA ZAWADI YA MAPINDUZI CUP ZIKO WAPI?

      Delete
  2. HIVI LILW GOLI KAFUNGA SARPONG AU KASEKE? MBONA HATUELEWI

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic