BAADA ya kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya AS Vita Club kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi, leo kinatarajiwa kuanza safari ya kurejea Bongo.
Bao pekee la ushindi kwa Simba lilipachikwa na mshambuliaji Chris Mugalu dakika ya 60 kwa mkwaju wa penalti uliosababishwa na Luis Miquissone dakika ya 59.
Leo Februari 13 kikosi kinatarajia kuanza safari mchana ambapo kikosi pamoja na benchi la ufundi watapitia Ethiopia.
Kesho Jumapili, Februari 14 saa 6 mchana kitatua rasmi ardhi ya Bongo ili kuedelea na maandalizi ya Ligi Kuu Bara pamoja na mechi za kimataifa.
Kundi A kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kituo kinachofuata ni Al Ahly, mchezo unaotarajiwa kuchezwa Februari 23, Uwanja wa Mkapa.
Big up Sana simba.mmetuwakilisha vema
ReplyDeletekusema kweli hongera mtani bila kinyongo sina ushabiki wa mhemko huu ni mpira na kuna burudani na upendo na sio uhasama mtu akifanya vizuri inapaswa apongezwe
ReplyDeleteTunashukuru mtani, na nyie mkiingia mkiweza kufanya Kama hivi Basi soka letu litapiga hatua maana vilabu hivi vikipata mafanikio vikiwa vikubwa ni rahisi hata ukizalisha vipaji na kufanya biashara kubwa ya kuuza wachezaji na pia kuwa wachezaji hodari wa timu ya taifa
ReplyDeleteSimba oyee kweli sku tukishiliki watani wajadi kwa pamoja itakuwa poa sana kweli
ReplyDeleteDah leonimeamin kumbe wapo na wana yanga wenye rohonzri Asanten
ReplyDeleteNimependa Sana maoni yenu na pia mlivyoonyesha uzalendo bila kuweka uyanga wala usimba ,pia niipongeze club ya Simba kujitahid na kupata point tatu muhimu tena ugenini ni jambo la kumshukuru Mungu kwakweli maana siyo kazi ya kitoto kuchomoka pale Congo bila mkono , mwenyenzi Mungu aitangulie timu ya Simba kwenye kila mchezo watakoucheza waweze kuibuka na ushindi amen
ReplyDelete