February 13, 2021


 KIKOSI cha Namungo FC kimezuiliwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Luanda, nchini Angola baada ya mamlaka kudai wachezaji watatu na kiongozi mmoja wana virusi vya Corona.


Mpaka wakati wa kuandika taarifa hii timu ipo uwanja wa ndege huku utata ukitawala kutokana na mamlaka za nchi hiyo kutaka msafara mzima ama urudi Tanzania au uende karantini.

Namungo ipo Angola kwa ajili ya kuchuana na Clube Desportivo 1º de Agosto katika mechi ya Kombe la Shirikisho.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kesho, Februari 14 na kikosi kilikwea pipa jana kikiwa na msafara wa wachezaji 22 pamoja na viongozi.

4 COMMENTS:

  1. Wameanza sisi tutamaliza kwa kishindo kikubwa.Tutawaambia wana Corona ya ajabu ajabu warudi walikotoka

    ReplyDelete
  2. Wametoka hapa hawana korona ila huko waneonekana na korona. So mbaya tutalipiza uzuri tunaazia kwao

    ReplyDelete
  3. Wanasahau kuwa na wao watakuja.Afrika bana akili zetu tunazijua wenyewe

    ReplyDelete
  4. Hiyo mbona simple, wakija hapa wapata kile kile, ngoma droo. Itabidi utafutwe uwanja neutral. Akili yetu waafrika ni mbaya, sasa kama watatu wana vorona, si waruhusu hao waliobaki? Ina maana nchini kwao hakuna waangola wenye corona, au wote wako karantine?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic