February 11, 2021

 


KIKOSI cha Azam FC kinachonolewa na George Lwandamina leo Februari 11 kimepoteza mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Coastal Union kwa kufungwa mabao 2-1.


Haji Ugando nyota wa Coastal Union alikuwa wa kwanza kumtungua mlinda mlango wa Azam FC, Mathias Kigonya,'Mikono Mia' kwa mkwaju wa penalti dakika ya 9.


Daniel Amoah aliweka usawa bao hilo dakika ya 34 na kuwafanya waende vyumba vya kubadilishia nguo ubao wa pale Tanga ukisoma 1-1.


Bao la ushindi kwa Coastal Union ya Juma Mgunda lilipachikwa dakika ya 54 na Rajab Majimengi na kuwafanya Azam FC wasiwe na mengi ya kufanya ndani ya Uwanja wa Mkwakwani.


Mchezo huo umechezwa Uwanja wa Mkwakwani,Tanga hivyo leo Coastal Union wamelipa kisasi kwa kuwa mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Azam Complex,  Coastal Union ilifungwa mabao 2-0.

Shujaa wa mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba, Kigonya ambaye aliokoa penalti ya Clatous Chama Uwanja wa Mkapa leo ameshindwa kuokoa penalti ya shujaa Ugando wa Coastal Union. 

Ushindi huo unaifanya Coastal Union kufikisha jumla ya pointi 23 ipo nafasi tisa huku Azam FC ikibaki na pointi zake 33 zote zikiwa zimecheza jumla ya mechi 19.

7 COMMENTS:

  1. Dah, Azam FC imegeuka kuwa kama timu ndogo zinazokamia timu kubwa. Hii ni aibu sana kwa wana lambalamba

    ReplyDelete
    Replies
    1. Azam namna gani ushindi wa sare dhidi ya Simba umewafanya kuvimba kichwa mpaka wanapoteza kwa kibonde. Yaani Azam walidharau kuloga kwakuwa ni coastal Union?

      Delete
  2. Leo azam hawakustahili kushinda kama wanavyoongea iongozi wao na vp iddy nado alishindwa kuwajulia mabeki wa coastal

    ReplyDelete
    Replies
    1. Jambo lao limeisha si wametoa droo na Simba we uoni walivyoshangilia nchi watu walikuwa wanajadili droo ya Simba kweli Simba noma

      Delete
  3. Azam jambo lao si ubingwa tena ila ni kutoka droo na Simba tu inawatosha na ndo thamani ya uwekezaji mkubwa walioufanya

    ReplyDelete
  4. Si huyo tu hata na wewe jirani jiangalie sana, usijisahau kwavile unajiita mwana......tayari unaongoza ligi ukadhan umeshachukua ubingwa bado, lolote linaweza tokea ndani ya mechi zilizobaki.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hilo ni dua la mwewe, subiri kwanza leo usiku uukalie ukishaandaliwa ukarudi hapa zitapenya kama umetia bamia

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic