MSAFARA wa watu 38 ukiwa na wachezaji 24 wa Yanga na viongozi 14 wa timu hiyo, leo Alhamisi utasafiri ku-wafuata Mbeya City kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa wikiendi hii.
Katika msafara huo, kiungo mshambuliaji raia wa Burundi, Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’ ameachwa jijini Dar akipewa program maalum kutokana na kutokuwa fiti ambapo hivi sasa anafanya mazoezi ya gym.Timu hizo zinatarajiwa kuvaana keshokutwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya ukiwa ni mchezo wa mzunguko wa pili.
Akizungumza na Spoti Xtra, Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Haji Mfikirwa, alisema kuwa maandalizi kuelekea mchezo huo yamekamilika na kikubwa wanakwenda Mbeya kufuata pointi tatu lengo likiwa ni kuendelea kukaa kileleni katika msimamo wa ligi.
Mfikirwa alisema timu hiyo inatarajiwa kusafiri leo alfajiri kwa ndege ambapo wameamua kutumia usafiri huo ili kutowachosha wachezaji kutokana na umbali wa safari hiyo.
“Maandalizi ya mchezo yamekamilika na msafara wetu utakuwa wa watu 38, kati ya yao wachezaji 24 na viongozi 14 watakaosafiri na timu,” alisema Mfikirwa huku akiwataja wachezaji watakaosafiri ni;Metacha Mnata, Farouk Shikalo, Mukoko Tonombe, Lamine Moro, Tuisila Kisinda, Bakari Mwamnyeto, Waziri Junior, Zawadi Mauya, Kibwana Shomari, Yassin Mustapha, Deus Kaseke na Farid Mussa.Wengine ni Said Makapu, Adeyum Saleh, Paul Godfrey ‘Boxer’, Omari Chibada, Dickson Job, Ditram Nchimbi, Yacouba Songne, Fiston Abdoul Razack, Haruna Niyonzima, Michael Sarpong, Feisal Salum na Carlos Carlinhos.
#Daima mbele #Daima kileleni #Daima uongozini.
ReplyDeleteNi kwa muda tu,mwenye nafasi yake yuko busy na majukumu ya kimataifa
Delete#Daima vidimbwini
ReplyDelete#Daima matopeni #Daima mchangani #Daima utopolo
ReplyDeleteYaa kaenda kushughurikiwa
ReplyDeletePandeni kimbinyiko mme wenu anaenda kuwatafutia nafasi wewe mke Ni legelege hujiwezi kujibeba
DeleteWanaume mashupavu wa Yanga yetu wameondoka kamili kwenda kupambana na timu ngumu huko Mbeya na wameapa kwa ushindi na huku tukiomba wapokewe kwa shangwe na huku wakitaraji wachezaji wetu dau nono pindi watapoishinda hiyo timu shupavu kwahivo mashabiki wasisahau kuipokea timu yetu wakiwemuo akina Niyamanzo na Saidooo kuinyima mikia Sports ubingwa. Kila la heri
ReplyDeleteDaima mbele nyuma mwiko
ReplyDeleteWatapata tabu sana
Mungu ibariki yanga
ReplyDeleteMuch blesses to you chama la wana
ReplyDelete