February 21, 2021

 


DITRAM Nchimbi,  mshambuliaji wa Yanga, leo Februari 20 ametimiza mwaka mmoja kucheza bila kufunga.


Mara ya mwisho ndani ya Ligi Kuu Bara alifunga mabao mawili Februari 20, Uwanja wa Mkapa kwa pasi za David Molinga.


Kwa sasa Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze ikiwa imefunga mabao 34 yeye amehusika katika mabao mawili ambayo alitoa pasi za mabao.


Pasi ya kwanza alimpa Michael Sarpong mbele ya Biashara United,  Uwanja wa Karume, Mara na ya pili alitoa mbele ya Kagera Sugar kwa Tonombe Mukoko.

Hivyo leo anatimiza mwaka mmoja bila kufunga ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara. 

4 COMMENTS:

  1. Halafu watu wanashangaa akikosa goli.Ni kawaida yake.Hamna hujuma wala vitisho.Chezeni mpira acheni kudeka.

    ReplyDelete
  2. Kufunga Kwaresma au saumu mbona kila beki anajua Moto wake Dada JIONGEZE?

    ReplyDelete
  3. Usidanganye na Takwimu za like Adamu,Bocco ,Kagere always wanapata Magoli ki Bonanza mechi moja goli nne

    ReplyDelete
  4. Tunahoji hata Elimu zenu pls kwa hii taarifa hiii ni matokeo ya FFFF

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic