February 14, 2021


 
UONGOZI wa Klabu ya KMC umesema kuwa Uwanja wa Nelson Mandela ulikuwa kikwazo kwao kupata pointi tatu kwa kuwa walifanya mazoezi ukiwa umejaa maji jambo lililowapa ugumu kupata matokeo.

Kwenye mchezo wa mzunguko wa Ligi Kuu Bara uliochezwa juzi, KMC ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 na Prisons na kuwafanya waache pointi tatu jumla ugenini.

 Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa walishindwa kupata pointi tatu kutokana na miundombinu kutokuwa rafiki kwao licha ya ubora wa kikosi chao.

“Tulikuwa ugenini hatukuweza kupata ushindi ipo wazi licha ya kwamba kikosi chetu ni imara na kinacheza kwa kujiamini.Hatujakata tamaa tunarejea kujipanga dhidi ya Mwadui FC,Februari 16.

“Uwanja haukuwa mzuri, tangu tumefika mvua zilikuwa zinanyesha na uwanja ulikuwa umejaa maji jambo ambalo lilifanya wachezaji washindwe kuonyesha kiwango kizuri, wapinzani wetu wamepata nafasi na wamezitumia hivyo wanastahili pongezi,”.

 Mchezo wa wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Uhuru, KMC iliyo nafasi ya 6 na pointi 25 ilishinda mabao 2-1 hivyo Prisons iliyo nafasi ya 7 na pointi 25 imelipa kisasi nyumbani kwa ushindi wa mabao 2-1.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic