February 14, 2021



UONGOZI wa Yanga umesema kuwa upo imara hauna presha katika kutimiza jambo lao la kuutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara, msimu wa 2020/21 ulio mikononi mwa Simba.

 Jana ilikuwa na kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Mbeya City, kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya na iligawana pointi mojamoja.

Bao la Yanga lilifungwa na Deus Kaseke dakika ya 84 lilionekana kulalamikiwa na wachezaji wa Mbeya City huku lile la kuweka usawa kwa Mbeya City lilifungwa dakika ya 90+3 na Athas Pastory kwa mkwaju wa penalti ambao ulilalamikiwa na wachezaji wa Yanga.

Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa wamejipanga kufanya vizuri kwa msimu huu wa 2020/21 hivyo mashabiki wasiwe na presha.

“Tupo imara hatuna presha katika yale ambayo tunayafanya, imani yetu ni kwamba tutapata matokeo chanya kwenye mechi zetu zilizobaki na kupata pointi tatu muhimu.


“Kikubwa mashabiki waendelee kutupa sapoti kwa kuwa wachezaji pamoja na benchi la ufundi limekubaliana kufanya kazi kwa juhudi hicho ndicho ambacho tunakifanya kwa sasa ndani ya uwanja,” amesema.

Yanga imekusanya jumla ya pointi 45 ipo nafasi ya kwanza na imecheza jumla ya mechi 19, Mbeya City ipo nafasi ya 17 na ina pointi 15 baada ya kucheza jumla ya mechi 19. 

Ikiwa imefunga jumla ya mabao 30, Michael Sarpong ametupia mabao manne, Wazir Junior ametupia bao moja huku Saido Ntibanzokiza akiwa ametupia mabao mawili.

Kinara wa utupiaji ni Deus Kaseke mwenye mabao matano ndani ya Yanga inayonolewa na Cedric Kaze.

10 COMMENTS:

  1. Mkifungwa mnaanza kuwazonga marefa, subirini rungu la tff kwa kocha wenu na mchawi wenu kaseke

    ReplyDelete
  2. Mnajifariji tu ila presha mnayo tena kubwa tu

    ReplyDelete
  3. Mbona mikia aka pk mweusi bado mna mechi nyingi tu za nje? Tusibiri

    ReplyDelete
  4. Timu zote mechi za ndani na nje idadi ni sawa

    ReplyDelete
  5. Yajayo yanafurahisha kwa Simba, maana mmesuburi sana lakini dua lenu hakijafanikiwa, labda la kuwauliza ni kuwa watakapokuja VITA mtawapokea kama desturi yenu isiyokuwa na mashiko?

    ReplyDelete
  6. Yajayo yanafurahisha kwa Simba, niwaulize watakapokuja VITA mtawapokea kama ilivyo desturi yenu?, Timu zote zilizokuja kucheza na Simba wapokeaji mlikuwa nyie, japo wakati wa kuondoka huwa hamwasindikizi kwakuwa wanakuwa wakula za uso, wanaondoka na manundu ya magoli, nyie maumivu mnabaki nayo, mnafikiria muda na gharama mlizotumia. Mpira uwanjani nje ya uwanja yanabaki maneno tu kama mnavyofanya nyie wa
    Matopeni ushindi kazi si blaaablaaa zenu

    ReplyDelete
  7. Yanga wapo vizuri no Hali tu ya mchezo naamini watasahihisha makosa yao na kuanza kupata matokeo

    ReplyDelete
  8. Mmeanza visingizio vya marefa chezeni mpira acha kulaumu, ndo mmeanza kuwazonga marefa itafika wakati mwingine mtawapika maana ni jadi yenu. Kisa sare

    ReplyDelete
  9. Mpira sio vita ni burudan, kama yanga itachukua itakuwa vizuri, na ikiukosa ubingwa wakubali tu pia

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic