FISTON Abdoul Razack, mshambuliaji mpya ndani ya kikosi cha Yanga amesema kuwa anaamini atafanya kazi yake ya kufunga mabao kwa ushirikiano na wachezaji wenzake ndani ya timu hiyo.
Nyota huyo ni ingizo jipya kwenye dirisha dogo ambapo alisaini dili la miezi sita akitokea Klabu ya ENPPI ya Misri na anatajwa kuwa mtatuzi wa tatizo la ubutu wa safu ya ushambuliaji wa Yanga.
Safu ya Yanga kwa upande wa ushambuliaji inaongozwa na Deus Kaseke mwenye mabao matano na ana pasi moja huku nyota Michael Sarpong na Yacouba Songne wakiwa wametupia mabao mannemanne.
Ikiwa imecheza jumla ya mechi 19 imefunga jumla ya mabao 30 na imefungwa mabao nane, ipo nafasi ya kwanza na pointi zake kibindoni ni 45.
Imewaacha kwa pointi sita watani zake wa jadi, Simba ambao wapo nafasi ya pili na pointi 39 baada ya kucheza mechi 17.
Fiston tayari amecheza mechi moja ya Ligi Kuu Bara ilikuwa mbele ya Mbeya City kwenye sare ya kufungana bao 1-1 na pia amecheza mchezo mmoja wa kirafiki ilikuwa wakati Yanga ikipoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya African Sports ya Tanga.
Nyota huyo amesema:"Nimeona wachezaji ni wazuri na wanapenda kupata matokeo ndani ya uwanja hivyo nami nitashirikiana nao kupata matokeo chanya na kufunga mabao pale ambapo ninapata nafasi.
"Ushindani ni mkubwa na kila timu inahitaji kupata matokeo chanya ndani ya uwanja, bado tuna muda wa kufanya vizuri na mashabiki watapenda wenyewe," amesema.
Kesho Febbruari 17, Yanga itakuwa na kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Kagera Sugar ya Mecky Maxime iliyo nafasi ya 10 na pointi 23, Uwanja wa Mkapa.
Mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja wa Kaitaba, Kagera Sugar ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 hivyo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Kwa mtazamo wangu, baadhi ya waandishi/magazeti mnawapamba mno wachezaji na kuweka matarajio makubwa kwa mashabiki kuliko uwezo halisi wa wachezaji bila kujali uhalisia kuhitaji muda wa ku--cope na mfumo wa timu a kuizoea ligi. Matokeo yake mnawapamba pressure wachezaji na kushindwa ku-perform kwa viwango mnavyowasifia...!
ReplyDeleteHuu usajili tunaoona una mashaka umefanywa na GSM bila kuushirikisha uongozi, kila mara tunaona GSM mara wapo DRC, mara Zambia, mara Rwanda, mara Angola, wanafuata wachezaji. Ni nani amewapa ninyi GSM mamlaka ya kuiongoza Yanga? Mnaona sasa aina ya wachezaji mliotuletea? Yaani kila mara tunatamani liwepo dirisha la usajili tuwaache walioletwa na GSM, ni hakuna kitu kabisa. Hii timu ni ya wanachama na ina uongozi uliochaguliwa na wanachama. GSM ni muwekezaji tu na mipaka yake inaishia kwenye mauzo ya jezi. Kama ana nia njema ya kuiinua Yanga basi atoe msaada kwa uongozi halali ili wao ndio waamue kuelekeza fedha mahali panapostahili, lakini sio sawa kabisa GSM kujitwalia mamlaka yaliyo nje na mkataba wa uwekezaji wake, inawafanya viongozi washindwe kutekeleza mipango yao maana wakati mwingine inakuwa inagongana na mipango au malengo ya GSM
ReplyDeleteUtajiju na kisilan chako nenda na ww ukatafte tmu ya kuwekeza
DeleteWewe iache GSM ifanye yake mpuuzi kwanza wewe siyo Yanga nenda kaishauri Simba yako achana na Yanga
DeleteWw sio bure umetumwa na mikia na kinachokusumbueni ni wivu,hivi kama usajili wa GSM ni mbovu mbona timu inaongoza ligi na haijafungwa hadi ss?Yanga ya ss iko makini sana na msitarajie kama mtaivuruga,daima mbele nyuma mwiko.
DeleteWaandishi wa hii blog wamekubuhu kwa kutunga habari na kuwalisha watu maneno
ReplyDelete