BAADA ya Simba kumalizana na AS Vita kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kwa sasa hesabu zao ni kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Biashara United.
Chini ya Kocha Mkuu, Didier Gomes, Simba ilishinda bao 1-0 mbele ya AS Vita, jambo ambalo limewapa furaha mashabiki na benchi la ufundi kiujumla.
Bao hilo lilifungwa kwa mkwaju wa penalti na mshambuliaji, Chris Mugalu baada ya kiungo Luis Miquissone kusababisha penalti hiyo.
Gomes ambaye anajivunia uwepo wa mzawa Mzamiru Yassin ndani ya kikosi cha Simba amesema kuwa hesabu kubwa ni kupata pointi tatu kwenye mchezo huo muhimu.
"Ninatambua kwaba utakuwa mchezo mgumu na wenye ushindani ila wachezaji nimewaambia kwamba tunahitaji pointi tatu.
"Kikubwa ambacho kitaturejesha kwenye mstari ni ushindi hvyo ili tushinde lazima tupambane ndani ya uwanja, mashabiki wazidi kutupa sapoti," amesema.
Simba ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 39 baada ya kucheza mechi 17 inakutana na Biashara United ambayo ipo nafasi ya nne na pointi zake ni 32.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Februari 18, Uwanja wa Karume, Mara.
0 COMMENTS:
Post a Comment