February 19, 2021


 FISTON Abdoul Razack ingizo jipya ndani ya kikosi cha Yanga inaelezwa kuwa aliomba akae pembeni kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar, kutokana na presha za makelele za mashabiki wa Yanga.

Nyota huyo amecheza mchezo mmoja wa Ligi Kuu Bara, ilikuwa dhidi ya Mbeya City, kwenye sare ya kufungana bao 1-1.

Alicheza pia mchezo wa kirafiki dhidi ya African Sports wakati wakifungwa bao 1-0, Uwanja wa Azam Complex.

Habari kutoka kwa mtu wa karibu wa Yanga zimeeleza kuwa nyota huyo aliomba kutocheza mchezo huo ili aweze kurejea kwenye hali ya kawaida.

"Presha za mashabiki zimemfanya Fiston aombe kujiweka nje ya uwanja kwa muda ili arejee kwenye ubora wake.

"Jambo hilo lilimfanya akae pembeni kwani kwenye mechi mbili amekutana na joto ya jiwe la mashabiki ambao wamekuwa wakimlaumu kwa kushindwa kuipa timu hiyo matokeo," ilieleza taarifa hiyo.

Cedric Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa bado Fiston anahitaji muda wa kuweza kuzoeana na wachezaji pamoja na kuwa kwenye ubora wake.

"Ninatambua uwezo wa Fiston ambaye ni mchezaji mpya kadri siku ambavyo zinakwenda anazidi kuimarika hivyo nina amini kwamba atarejea kwenye ubora wake,".

Yanga ikiwa ipo nafasi ya kwanza kesho ina kazi ya kumenyana na Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa ligi ambao ni mzunguko wa pili.

Mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Yanga ilishinda bao 1-0 hivyo kesho utakuwa mchezo mkali kwa timu zote kusaka pointi tatu.

7 COMMENTS:

  1. Alisifiwa sana na Kocha mwenyewe na magazeti ya michezo yakampamba kila siku ukurasa wa mbele na picha yake, matokeo yake ndio hayo matarajio ya washabiki na wapenzi yalichagizwa mnoo na sifa alizopewa kabla na baada ya kuja... Tunahitaji matokeo uwanjani na sio nje ya uwanja haswa magazetini na mitandaoni...

    ReplyDelete
  2. Utopolo mmezoea mpira wa magazetini na mitandaoni.

    ReplyDelete
  3. Kutoka kuitwa mtambo wa mabao mpaka kuitwa ingizo jipya.... Tuliwaambia punguzeni maneno fanyeni kazi kwanza lakini hamkujali. Mpira hauchezwi mdomoni Wala magazetini, jifunzeni kwa MNYAMA oneni navyoendesha mambo yake kisasa japo mnamkejeli lakini anasonga mbele na msipo kuwa makini mtakuja kushtuka atakuwa ameshawaacha sana

    ReplyDelete
  4. Simba nyote makuma tu na we mwandishi ni mavi ya mama yako maana huna source of information yako

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sasa matusi yote haya ya nini? Inaelekea wewe si mpenzi wa mpira maana si kwa matusi hayo

      Delete
  5. Hii habari ya kuwasifia wachezaji bila kuwaona madhara yake ndyo haya, Miquisone na Ntibazonkiza kwa mfano, walifika na kukiwasha lakini hawa wengine tunasema hadi wazoee huku ligi inaendelea ni hasara. Huyo ni garasa tuambiane ukweli tu kama akina Wilker Da Silva na sisi tulipigwa

    ReplyDelete
  6. Hivi kwa nini mtu utukane mashabiki wote wa simba? Huo ni utovu wa nidhamu. Simba kuna watu wengi na wa aina zote. Chunga sana wewe jamaa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic