February 19, 2021

 


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa ikiwa waamuzi wa mchezo wao wa kesho wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar watashindwa kuchezesha kwa haki na kuwanyima penalti ndani ya dakika 90 wataomba kujiondoa kwenye ligi.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa wamekuwa wakionewa mara nyingi ndani ya uwanja na wanakaa kimya jambo ambalo linawaumiza.

Makamu huyo amesema:"Tulikuwa na mchezo dhidi ya Mbeya City kwenye sare ya kufungana bao 1-1, tulinyimwa penalti ya wazi ila mwamuzi aliwapa Mbeya City penalti pia, licha ya kuongea hilo hakuna hatua iliyochukuliwa na tumebaki tukionewa.

"Pia mchezo wetu dhidi ya Kagera Sugar kwenye sare ya kufungana mabao 3-3, tulinyimwa penalti ya wazi ambayo imetufanya tushindwe kufanya vizuri ndani ya uwanja.

"Mashabiki wetu wamekuwa wakikanywa na kusababisha tupigwe faini kwa wakati bila kusubiri ikiwa ni laki tano, laki tatu sasa hili  hatukubali ikiwa haki haitatendeka kwenye mchezo wetu wa kesho, tunaweza kuomba kujitoa kwenye ligi.

"Kikubwa tunahitaji haki ndani ya uwanja, kwani mashabiki wetu wanapenda kuona timu ikifanya vizuri ila pale ambapo wanashindwa kuona seheria 17 zinafuatwa basi wanakuwa na maamuzi ambayo yanasababisha tupigwe faini," . 

9 COMMENTS:

  1. Kwa kua hamjawahi kufungwa msimu huu tunawasubiria kesho mfungwe halafu mjitoe mchana kweupeee....

    ReplyDelete
    Replies
    1. Utopolo wamezoea kubebwa kwa kupewa penalty za ajabu kumbuka penalty waliyopewa dhidi ya Simba ambapo faulo ilifanyikia nje ya 18 lakini refa akawazawadia penalty

      Delete
  2. Serious!!!!! Kiongozi mkubwa aliyewahi kuongoza shirikisho la soka anaweza kuongea pumba kama hizi!!!!

    ReplyDelete
  3. Kwa hiyo kesho wanajua kutakuwa na penalti?
    Utopolo kweli safari hii mmepata viongozi mizigo.

    ReplyDelete
  4. Anacheza na akili zawaamuzi ili kesho wawemakini ikitokea fursa ya penalty wapewe... vinginevyo hizo ni presha baada ya kudondosha pointi 6 mechi tatu zilizopita!

    Hata Simba walishanyimwa penalty mechi za huko nyuma kama dhidi ya Prisons...makosa ni makosa tu, kutishia kujitoa kwa klabu kubwa kama Yanga ni aibu!

    ReplyDelete
  5. WAJITOE TU, WANAWEZA KULIPA ZA WADHAMINI WAO? WAMEKULA HELA ZA SPORTS. GSM, NA WENGINEO UNADHANI UBAVU WANAO, SARE NYINGINE INAFUATA

    ReplyDelete
  6. Kwa hiyo wanaomba kesho wapewe penati hata kama haistahili, kisa watajitoa, basi watoke tuu

    ReplyDelete
  7. Wajitoe waunde ligi Yao "vpl hamna vya bure pambaneni kubebwa hakupo

    ReplyDelete
  8. Anasema iwapo refa atawanyima penati, anajuaje kama watapata penati? :d
    Au kila mechi lazima Yanga wapate penati? Mbona sielewi hii?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic