February 10, 2021

 

KOCHA mkuu wa klabu ya Simba, Didier Gomes amejiandaa kuwasapraizi wapinzani wao AS Vita katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba na AS Vita ya DR Congo, kwa kuwapa nafasi baadhi ya nyota ambao hawakuonekana katika michezo yao iliyopita.

Mchezo huo wa kwanza wa kundi A, unatarajiwa kupigwa katika dimba la Martyrs, uliopo Kinshasa nchini Congo majira ya saa 11 jioni kwa saa za DR Congo ambayo ni sawa na saa 1:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Simba iliondoka jana saa 10 jioni uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar ikiwa na wachezaji wake wote mahiri akiwemo kiungo Jonas Mkude na tayari wameshatua jijjini Kinshasa,
Congo.

Akizungumzia mipango yao kuelekea mchezo huo Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes Da Rosa amesema: “Tumejiandaa vizuri na mchezo wetu wa kwanza wa hatua ya makundi dhidi ya AS Vita, tunajua hautakuwa mchezo rahisi kutokana na ubora wa wapinzani, lakini tumejipanga kukabiliana na hali hiyo ili kuweza kupata ushindi katika mchezo huo.

“Kuelekea mchezo huo tutakuwa na sapraizi ndani ya kikosi chetu, ambapo kutakuwa na mabadiliko ya baadhi ya wachezaji ambao hawakucheza michezo iliyopita.


11 COMMENTS:

  1. Mnatuchanganya, wekeni vizuri suala la muda, ni saa moja au saa tatu usiku?

    ReplyDelete
  2. AZAM TV SAA 4:00 USIKU hatuelewi

    ReplyDelete
  3. Mchezo utapigwa saa mbili za usiku kwa saa za Congo na kwetu itakuwa saa nne usiku

    ReplyDelete
  4. Weken wachezaji wa sapraiz muone hicho kipigo chake, mtapigwa kumi bila

    ReplyDelete
    Replies
    1. Endelea kuota hivyo hivyo ndoto za alinacha we unafikiri Kila siku Jumapiki,au unafikiri Simba ni Kama Utopolo,endelea kuomba mabaya kwa Simba lkn utaishia kuondoka na majonzi na aibu shuuuuu wendawazimu nyinyi

      Delete
  5. Utopolo inakuhusu nini?Ngoma ya wanaume Kachezeni vigodoro na African Sports.

    ReplyDelete
  6. Hakuna cha surprise hapa ni kipigo tu nguruwe fc nyie

    ReplyDelete
    Replies
    1. We nyani FC maneno hayauwi alafu sisi Simba sio saizi yenu Ila mnalazimisha kuongea na sisi nyie kachezeni mnapochezaga na African Sports,alafu kaa kwenye angalia wake zenu AS Vita wanavyopasuka hapo hapo kwao Ila hatutaki uzimie manake ndio Tabia zenu Kidimbwi fc

      Delete
  7. Ni wame zao sio wake zao nilikosea,maana As Vita wake zao si yanga huoni wanavyowashobokea, Yani Vita hata wakitaka kussuza Rungu kwa Yanga,Chura FC lazima wabinue Chura juu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic