February 10, 2021

 

KOCHA Mkuu wa AS Vita ya DR Congo, Florent Ibenge amesema kuwa anaamini kama wachezaji  Clatous Chama na Jonas Mkude watacheza kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi yao siku ya Ijumaa basi watapata wakati mgumu katika mchezo huo.

Mara ya mwisho kwa Simba na AS Vita kukutana, Simba ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, huku bao la ushindi la Simba likifungwa na Clatous Chama katika mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Mkapa jijini Dar.

Mkude pia alikuwa sehemu ya kikosi cha Simba ambacho kilicheza na Vita katika mechi ya kwanza nchini Congo ambapo Simba walipoteza kwa mabao 5-0.

Akizungumzia maandalizi yao kuelekea mchezo huo, Ibenge amesema “Nawakumbuka wachezaji wengi wazuri ndani ya kikosi cha Simba kama Clatous Chama na Jonas Mkude, kwenye mchezo wetu wa mwisho dhidi yao ambao tulipoteza, nakumbuka Chama ndiye alitufunga bao lililotutoa kwenye mashindano.“

"Lakini pia namkumbuka Mkude alicheza vizuri, nadhani wachezaji hao wanahitaji ulinzi zaidi ili wasitupe madhara kuelekea mchezo huu ambao tutakuwa nyumbani.“

 

 

5 COMMENTS:

  1. akili yako finyu kweli..
    usidhani kwa kuandika kuwa Nado amesema hivi, Walter Bwalya amesema hivi, au Ibenge amesema hivi ndiyo basi watu wataamini... Wenye akili huweka na source hata ikiwezekana link ya video, website kudhibitisha wamesema hivyo..maneno yako si chochote bali yanaonyesha upungufu wa akili yako.
    Mkude ana muda gani hajacheza? inakuwaje anaogopesha...lofa kweli

    ReplyDelete
  2. Pumbavu sana et Ebenge atishiwe na mkude na CHAMA! Ina maana kipindi kile wanakula 5-0 hawakuwemo? Ukikosa cha kuandika nenda ukakojoe arafu ulale

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe ndo chizi kwani walivyoenda Dar aliyewafunga goli la pili Nani,tatizo washabiki wa Yanga wengi ni mambumbu Mpira hawajui,wanaofikiri game ya 5-0 Basi na game hii itakuwa hivyo hivyo,Kama ni hivyo Basi ata Al Ahly asingemtoa Mamelodi mwaka Jana maana mwaka juzi alifungwa 6-0 Tena robo fainali,Sasa chuki za utopolo za kusema hamsa hamsa wkt Kuna timu msimu Simba anafungwa tano yenyewe ukifungwa 8-0 lakini uwasikii kuongelea hiyo,waache wandelee na chuki zao dhidi ya Simba alafu watabakia hapo hapo Kila siku WEHU nyinyi

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic