February 18, 2021


 KILA kitu kinakwenda kwa namna ambavyo unapanga na kupambana ili kuona mwisho wa siku unapata matokeo ya kile ambacho unakihitaji.

Ila inabidi ukumbuke kufanya kazi kwa juhudi ni jukumu lako ila suala la mafanikio muachie Mungu kwa kuwa yeye anajua namna ya kugawa riziki.

Hapo ndipo ambapo imekuwa ni mtihani kwa baadhi ya wachezaji linapofika suala la kukubali matokeo ndani ya uwanja.

Hali hiyo pia imeambukizwa mpaka kwa mashabiki nao wana kasumba ya kugoma kukubali matokeo ndani ya uwanja baada ya dakika 90.

Tatizo limezidi kuwa kubwa si kwa Yanga, Simba,KMC Lipuli mpaka Njombe Mji unaambiwa hakuna ambaye anakubali matokeo ya aina yoyote kwa pande hizi mbili.

Nakumbuka Simba ilishinda mabao 4-0 dhidi ya JKT Tanzania, baada ya dakika 90 kuisha mashabiki kama kawaida walianza kusikitika kweli na kusema ilikuwa mtu apigwe nane, sema wachezaji walijisahau na kuanza kupiga pasi nyingi.

Weka kando hiyo Simba ilipopoteza mechi mbili mfululizo mbele ya Tanzania Prisons kisha ikapoteza mbele ya Ruvu Shooting, maneno. Hakuna shabiki ambaye alikubali matokeo.

Wakaanza Clatous Chama hayupo sasa timu inarukaruka tu, mfumo wa mwalimu mbovu yaani ilimradi tu hakuna anayekubali matokeo.

Njoo kwa ndugu zetu KMC wazee wa pira spana, walipokutana na wale Wajelajela, Tanzania Prisons na kupoteza kwa kufungwa mabao 2-1, unaambiwa matokeo hayo yalisababishwa na mvua kunyesha jambo lililowafanya wasiwe na namna wachezaji kusaka ushindi.

Sare ya bao 1-1 waliyopata Yanga mbele ya Mbeya City,wachezaji walivimba kila mmoja anataka kumvamia mwamuzi sasa sijui walitaka kumfanya nini wanajua wenyewe.

Lamine Moro ilibidi abadilishe majukumu na kuwa mlinzi wa mwamuzi, mashabiki nao sasa kama kawaida kwao kurusha makopo ni kawaida. Muda wa ugomvi uwanjani umekwisha kwa sasa.

Matokeo yake ni kwamba vurugu hizo zimewafanya Yanga watozwe faini ya laki tano ambayo haikuwa na ulazima wa kufanya hivyo kwa namna yoyote ile, mpira ni ndani ya uwanja.

Hatukatai kwamba ni lazima kuongea pale matokeo yanapokuwa mabovu hata mazuri ila ni muhimu kuwa na mipaka na nidhamu katika kuzungumza na kuchukua sheria mikononi.

Kuna shabiki mwingine ameweka wazi kwamba anaweza kumdhuru mwamuzi, kisa sare. Naona hii sio sawa, mpira sio vita mpira ni burudani.

Zipo sababu ambazo zinasababisha timu ishindwe kupata matokeo, ubovu wa miundombinu ni sababu hasa kwa mazingira ya Tanzania, viwanja bora vinahesabika.

Ukianza na kwa Mkapa, Azam Complex,Uhuru, Kaitaba sasa hivyo vingine taratibu sehemu ya kuchezea haina ubora hivyo iwe somo kwa wamiliki wa timu kugandamizia mpango wa Azam FC kwa kumiliki uwanja wao wa kisasa.

Masuala ya kuleta vurugu na makelele baada ya mpira sio sawa kikubwa ni kuwa watulivu na kushangilia bila kuogopa. Wachezaji kazi yenu iwe moja kusaka ushindi ikitokea mkapata sare, mkapoteza ama mkashinda sawa.

Muhimu kwa kila timu kuweza kuwa na maandalizi mazuri, mzunguko wa pili una ushindani mkubwa na kila timu inahitaji ushindi.

Ikiwa kila siku unataka timu yako ishinde sasa timu ya nani unataka ishindwe na kwa nini?

7 COMMENTS:

  1. Wee tunakujua unakaunafika na mahaba Fulani.na huipendi yanga

    ReplyDelete
  2. Kwani kasema uongo?Wenye kutupa makopo ns kulalama wanajulikana.Hiyo haina viongozi?Au na wao wanatishiwa na kuondoka kwa escort ya Polisi!!!

    ReplyDelete
  3. Inaonesha wewe unajidanganys kuwa Yanga ni kipenzi cha kila mtu. Hapo kaka umeteleleza na ukishaipenda wewe Yanga na wenzako inatosha. Mimi binafsi hainivutii Yanga kutokana na kupenda fujo kama vile kulalamika kila wakati, kuzomeazomea kupiga na kuchana waungwana mashati yao

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tulia subiri dawa iingie vizuri....waamuzi nao waonje shubiri ya kuumizwa kwa kunyonga haki.....mashabiki wanaumia

      Delete
  4. Hongera kwa kuelezea changamoto hii inayotutafuna sisi wafuatiliaji wa mpira Tanzania, kiukweli tunakuwa na wakati mgumu pale timu inapokosa kujituma kwa nguvu na kupoteza mchezo, kutoka sare ama kushinda kwa ushindi mwembamba wakati nafasi zilikuwa zinaoneka kuwa wazi za kufunga magori mengi zaidi.Tunafurahi kuona timu zote zinapambana kusaka matokeo uwanjani, hatupendezwi na Vurugu uwanjani. Mpira ni furaha na Amani.

    ReplyDelete
  5. Inategemea na upeo na uelewa wa mtu ,mchezo wa Soka kwa wanaotambua Maadili yake kwa Ujumla,huwa hawapigi kelele,Wewe unaandika kuhidhinisha usanihi wa kisingizio Cha ustaarabu,.Lakini Watu wenye munkari ya Soka wapo Duniani kote na kila eneo husika lina changamoto zake ,.Nitoe mfano Ulaya Pana Ubaguzi wa rangi na Kamari bado ufumbuzi wake hata FIFA wameshindwa,Lakini kwa taarifa za wanaochukia ubaguzi watamtaja hata Rais wa FiFA kushiriki maadam wameruhusiwa kutoa maoni kwa mujibu wa nafasi zao na wana nafasi ya kutoa mawazo .Africa(Tanzania hasusani)kwenye Soka kutumia madaraka kwa maslahi binafsi kisingizio cha taratibu ni u Professor.Kwa mujibu wa sheria a Nchi mwizi akikamatwa akipigwa na kuuliwa na raia ni kuchukua Sheria mkononi na ni kosa kisheria .Hapo kibaka anapata nguvu ya kuiba akikurupushwa tu anakimbilia kinga ya Polisi japokuwa ukweli ni kwamba kaiba.Refa,Media Viongozi ni ukomavushi Kama siyo upevushi wa uharibifu wa maadili ya Soka kwa kisingizio Cha kulindwa na utaratibu wa mchezo huo.Kwa maana Hii inahitaji mapokeo yenye hisia maaria yenye kuzingatia utaratibu na uhalisia wa maisha .Tanzania kwetu kutumia raslimali au haki ya Umma kwa matumizi yako binafai unaitwa mjanja una akili nyingi.Sasa nimalize kwa kusema tuwe wa kweli na tulinde maadili ya Tathnia zetu Lakini tunapokengeuka kwa maksudi tuwe tayari kupokea matokeo maadam wote tumeendekeza hisia binafsi tukiweka mbali maadili.

    ReplyDelete
  6. Marefa , Waandishi siyo waadirifu inafika hatua hata mmiliki wa blog akiona maoni yapo nje ya mwelekeo/hisia zake ana comment kwa kutumia Unknown maadam kajificha kwenye Haki za Uhandishi wa habari,TCRA inatakiwa kusimamia njia za mawasiliano zote kila mtoa maoni ajulikane nataja Redio mfano Tumaini ,hata salamu lazima mtu ataje jina,na media za wenzetu ukitoa maoni unajulikana kwa jina halisi ,hapa UNKNOWN ni nyingi kwa sababu gani?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic