KOCHA Mkuu wa Mbeya City, Mathias Lule amesema kuwa watapambana kupata pointi tatu muhimu leo mbele ya Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Sokoine.
Ikiwa ipo nafasi ya 18 na pointi zake 14 baada ya kucheza jumla ya mechi 18 leo inawakaribisha vinara wa Ligi Kuu Bara, Yanga wenye pointi 44 na wamecheza jumla ya mechi 18.
Kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Yanga ilisepa na pointi tatu za Mbeya City mazima jambo ambalo leo litafanya mchezo huo uwe na ushindani mkubwa.
Akizungumza na Saleh Jembe, Lule amesema kuwa wanatambua wapinzani wao wanahitaji pointi tatu hata wao wanazihitaji pointi hizo ambazo ni muhimu.
"Wanakuja uwanjani kusaka pointi tatu, nasi pia tunahitaji pointi tatu ndani ya uwanja hivyo kazi yetu ni moja kutafuta ushindi.
"Tunawaheshimu wapinzani kwani ni muhimu kufanya hivyo hasa ukizingatia ni vinara wa ligi na ni timu kubwa hilo wanastahili ila kwa upande wa pointi nasi tunahitaji.
"Kikubwa maandalizi yetu sisi yapo vizuri na kila mchezaji anapenda kuona tunapata ushindi hilo lipo wazi mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti," amesema.
Kipa wao namba moja ni Haruni Mandanda ambaye Uwanja wa Mkapa alianza kikosi cha kwanza na jitahada zake ziligonga mwamba dakika za lala salama baada ya Lamine Moro kumtungua.
Ikiwa wamechapwa na African Sports isiyojulikana, vipi mshindwe nyie. kazeni buti tu
ReplyDelete