WAPINZANI wa Simba kwenye mchezo ujao kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi, Al Ahly ya Misri wameanza kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Al Merrik.
Mabao ya Al Ahly yalipachikwa na Mohamed Magdy dakika ya 57, Kahraba dakika ya 63 na Walter Bwalya dakika ya 71, Uwanja wa Cairo.
Ushindi huo unawafanya kwa sasa Al Ahly wawe vinara wa kundi A ambalo awali lilikuwa linaongozwa na Simba baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya AS Vita kwenye mchezo waliocheza ugenini.
Wanatarajiwa kukutana na Simba iliyo nafasi ya pili ila ina pointi tatu na bao moja Februari 23, kwenye mchezo wa hatua ya makundi Uwanja wa Mkapa.
Kwenye mchezo huo wakati wakishinda mabao hayo na kuonyesha balaa ndani ya uwanja, Al Ahly walipiga jumla ya mashuti 22 langoni kwa wapinzani wao Al Merrikh na katika hayo ni mashuti 6 yalilenga lango huku wapinzani wao walipiga jumla ya mashuti 8 na katika hayo manne yalilenga lango.
Umiliki wa mpira Al Ahly ilikuwa ni asilimia 71 na wapinzani wao asilimia 29 na walipiga jumla ya pasi 648 huku Al Merrikh walipiga jumla ya pasi 272 hivyo Simba wana kazi ya kufanya ndani ya kundi A.
Kwa hakika Al Marikh walikuwa under complete siege. Simba inabidi kesho katika mchezo wake na Biashara kikosi chake cha mwanzo kamili kujitayarisha kwa kimbunga cha Al Ahli. Mungu ibariki Simba
ReplyDeleteWalivyokuja Mara ya mwisho tuliambiwa Kuna mchezaji ana thamani ya bilioni 10,Mara 4 ya thamani ya kikosi kizima Cha Simba,Ila kilichotokea Mhh!!Sasa Tena washaanza kuwasifia kitakachowapata hapa kwa Mkapa andaeni kabisa visingizio vya kutosha
ReplyDeleteHawaijui simba, na baada ya matokeo wataleta visingizio kibao, maana hata mechi ya as vita wamesema kwamba as vita tuliyoifunga juzi sio ile ya kipindi kile, sasa sijui simba ni ileile, wajinga sana hawa watu yani hawakosi visingizio utaona itakavyokua.
ReplyDeleteMungu Yuko nasi Simba Sports Club ushindi ni lazima
ReplyDelete