February 12, 2021


 KITENDO cha nyota wa Azam FC, Idd Seleman, ‘Nado’ kumtungua Aishi Manula na kutoa pasi moja kwenye mchezo huo kwa mshikaji wake Ayoub Lyanga kunamfanya aingie anga za Yanga.

Nyota huyo mzawa mwenye machachari kutokea pembeni alifunga bao lake la nne pamoja na kutoa pasi yake ya nne ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2020/21.

Hivyo Nado amehusika kwenye mabao nane ndani ya Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina akiwa sawa na nyota wa Yanga, Yacouba Songne ambaye naye amehusika kwenye mabao nane.

Songne amefunga mabao manne na kutoa pasi nne kwa Yanga ambayo imefunga jumla ya mabao 29 huku Azam FC ikiwa imefunga jumla ya mabao 27.

Nado amesema kuwa furaha kubwa ni kuona timu inapata ushindi hivyo anaamini atazidi kupambana kufikia malengo yake pamoja na timu kiujumla.

"Kila mmoja anatambua kwamba tunahitaji ushindi hivyo tutazidi kupambana ili kupata matokeo ndani ya uwanja,".

Jana Azam FC iliacha pointi tatu mazima Uwanja wa Mkwakwani, Tanga baada ya kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Coastal Union.

5 COMMENTS:

  1. Pumba tupu.Waandishi makanjanja katika ubora wao

    ReplyDelete
  2. Nado ni mchezaji mpambanaji anastahili kuwepo Azam, Simba, Yanga na nje ya nchi hivyo yeye tu akiamua na kuangalia maslahi yake kwanza mpira ni Ajira. Namshauri alisibweteke akaze uzi na apambane zaidi atafika mbali kisoko.

    ReplyDelete
  3. Kuifinga simba ndio kigezo cha kusajiliwa? Hatuko serious kabisa.

    ReplyDelete
  4. Kwani si mlisema nyani fc wamefungiwa kusajili

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic