IKIWA leo Februari 12, Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, David Moyes itashuka Uwanja wa Mertedeys wa Congo kumenyana na Klabu ya AS Vita, wameweka wazi kuwa watashambulia na kujilinda kwa umakini.
AS Vita ni miongoni mwa timu bora ukanda wa Afrika ina ushindani mkubwa na Klabu ya TP Mazembe ambayo ilicheza na Simba kwenye Simba Super Cup na kulazimisha sare ya bila kufungana.
Tayari kikosi kimeshawasili Congo kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kuelekea kwenye mchezo huo wa kwanza kwa Simba msimu wa 2020/21.
Akizugumza na Saleh Jembe, kocha msaidizi wa Simba Seleman Matola amesema kuwa wataingia kwa nidhamu huku wakishambulia kwa hesabu pamoja na kujilinda kwa umakini.
“Kila mchezaji yupo tayari na tunajua kazi ni ngumu kimataifa ila hatuna mashaka kutokana na kuwa na muda wa maandalizi pamoja na ushirikiano ambao upo ndani ya timu.
“Ushindi ni mbinu ili ushinde ni lazima ushambulie hivyo tutashambulia kwa hesabu pia ni lazima tulinde lango letu ili liwe salama kwa kuwa ugenini inabaki kuwa ugenini,” amesema Matola.
Jana kikosi kimefanya mazoezi ya mwisho kwa ajili ya mchezo wa leo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Miongoni mwa nyota ambao wapo kwenye kikosi hicho ni pamoja na Jonas Mkude,Said Ndemla, Erasto Nyoni.
Mhh Simba inanolewa na David Moyes 😷😷😷huyu mwandishi ni kiboko aisee
ReplyDeleteHakuna waandishi humu bro'
DeleteHivi Saleh Ally haoni huu uzembe.Hamna proof reading?
ReplyDeleteHuu si uzembe ni kusudi watatuelewa tu na Didier Gomes
ReplyDelete