February 15, 2021

 


KUNDI A Ligi ya Mabingwa Afrika ni moto wa kuotea mbali kutokana na timu ambazo zipo kwenye kundi hilo kuwa zimewekeza kwenye wachezaji na uimara wa vikosi vyao.

Ndani ya kundi hilo ambalo linatajwa kufuatiliwa na wengi pia ipo timu kutoka ardhi ya Tanzania ambayo ni Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes mrithi wa mikoba ya Sven Vandenbroeck aliyebwaga manyanga, Januari 7,2021.


Wawakilishi hao wa Tanzania wana kazi kubwa ya kuboresha kikosi chao ili kupata matokeo chanya hasa kwa kuanza na sehemu ya ulinzi ambayo ipo chini ya Pascal Wawa na Joash Onyango ambao ni mabeki wa kati.

 Kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika wakati Simba ikishinda bao 1-0 dhidi ya AS Vita, njia ya kutokea kwa wapinzani ilikuwa kwa mwamba Mohamed Hussein,"Tshabalala' baada ya ule upande wa Shomari Kapombe kuonekana ni mgumu. 

Hali hiyo ilifanya kiungo Luis Miquissone kuongeza nguvu ya kuwa beki kwa kuwa alisababisha faulo moja na kona moja kutoka upande wa Mohamed, hapo Simba wanakazi ya kuboresha zaidi.

Ukitazama ushindani ulivyo pamoja na ratiba yao haitakuwa rahisi kufikia mafanikio bila jitihada, itazame namna ratiba ilivyo:-

Februari 23:-

Simba v Al Ahly 

Al Merrik v AS Vita 

Machi 5

Al Merrikh v Simba

Al Ahly v AS Vita

Aprili 2

Simba v AS Vita

Al Merrick v Al Ahly

April 9

Al Ahly v Simba

AS Vita v Al Merrick 


13 COMMENTS:

  1. Hujaweka mechi ya mwisho simba al mereck

    ReplyDelete
  2. Hakika Mohammed Husein amekuwa akiyumba hizi siku za karibuni hata kwenye mechi ya Azam.Simba wanatakiwa kulifanyia kazi tatizo hilo mapema. Awe anapewa nafasi Gabriel pia pengine ana vitu tofauti.shabalala anaonekana kuchoka pengine anahitaji kupumzika kidogo.

    ReplyDelete
  3. Lakini hawajafungwa wenye ulinzi mzuri wamedungwa ajabu sana

    ReplyDelete
  4. Ratiba yako haijakamilika, Simba vs. El merrekh hujaonesha!

    ReplyDelete
  5. Waandishi wa Utopolo wamekosa la kusema.Upande wa Mohamed Hussein ndio Vita walikuwa wanapeleka mashambulizi yao kupitia kwa Djupa Shabani kutokana na Simba kuwaruhusu washambulie zaidi kutokana na mfumo waliocheza.Djuma hutamuona Daressalaam kwenye mechi ya marudiano kwani Simba itatumia mfumo meingine.Luis hatarudi nyuma kumpa nafasi ya yeye kushambulia.
    Waandishi jifunzeni mifumo ya mpira kuliko kukariri.Mlitegemea matokeo tofauti hivyo "ego" zenu na kiburi haziwaruhusu kuandika ukweli.Badilikeni wacheni kukariri.

    ReplyDelete
  6. Ni kweli Shabalala sasa sasa hivi amekuwa uchochoro hata mechi nq azam ametugharimu sasa hivi watu wamefunguka kwanini aliachwa kikosi cha chan

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nafikiri Tshabalala amekuwa na hulka yakupanda sana mbele na hivyo kujichosha. Ni vizuri kocha akampuzisha Tshabalala na kumpa nafasi pia Michael Gadiel japo naye anakatika sana.

      Delete
  7. mfumo wa kocha 2 syo kwamb t shambalala ana ubovu wowote apana

    ReplyDelete
  8. Mimi we jamaaa sikuelewagi yaani. Unapost makala nyinginyingi zinazooenesha kuwa Simba hakujatulia muda wote. Za Chama Sasa umeachana nazo.sasa umeanza lingine.

    Hili la Mohamed Hussein linaweza kuwa Lina ukweli lakini generalization yako inawalakaini. Tambua unaandikia watu wengi. So zingatia taaluma yako na upenzi weka kando ili wasomaji wako tuendelee kukufuatilia.

    ReplyDelete
  9. Kama n uchochoro as vita walifunga magoli mangapi kuptia njia ya tshabalala?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic