February 15, 2021


 LICHA ya Uongozi wa Yanga kupitia kwa Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Hersi Said ambaye ni Injinia akiwa ni Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Kampuni ya GSM kukabidhiwa hesabu za fedha ambazo Yanga inadaiwa na Amissi Tambwe bado hajalipwa.

Staa huyo wa Burundi aliyekipiga ndani ya Yanga amesema kuwa bado hajalipwa fedha zake ambazo ni milioni 41 baada ya kufungua kesi FIfa kwa kile alichoeleza kuwa hakulipwa stahiki zake pamoja na fedha za usajili.

Fifa iliiamuru Yanga kulipa mkwanja huo kwa Tambwe ikiwa ni pamoja na malimbikizo ya posho na mshahara wake.

Tambwe amesema:-"Tumekamilisha kuwasilisha hesabu kwa mabosi ila mpaka sasa hakuna ujumbe niliopata kwamba fedha zimeingia ama na sielewi Yanga wamekwama wapi?.

"Sikuwa na lengo la kufika Fifa na wala sijafulia kama ambavyo wengi wanaeleza ukweli ni kwamba ninadai jasho langu na nilafanya kazi nikiwa ndani ya Yanga.

"Kwa kuwa jukumu lao nilitimiza kwa wakati hivyo nao ni jukumu lao kunilipa, ikiwa watashindwa sijui nini kitafuata kwani hilo jukumu ni lao na sio mimi tena,".

Hivi karibuni, Injinia Hersi alinukuliwa akisema kuwa watashugulikia suala hilo na kulipa kwa wakati.

4 COMMENTS:

  1. GSM kagoma kulipa deni lisilowahusu. Msindo na mwakalebela okoeni jahazi litazama. Adhabu itakayofuata ni kushushwa daraja hadi la nne

    ReplyDelete
  2. Hawa mstopolo sasa ni wwadaiwa sugu na wamekuwa kama debe lenye matundu, ukitia maji mara yanavuja yote. GSM anautilia mbolea mti ambao shina lake limeoza, uko wapi uhai hapo

    ReplyDelete
  3. ni ngumu sana hivi kwanini mambo haya ya kutolipana mishahara hayaishi ni jambo lakushangaza na la aibu kwa timu kubwa kama yanga inashindwa kumlipa chezaji mshahara wake mpaka inafikia hatua hii ya kufungiwa, hivi kweli kuna mshabiki yeyote wa mpira hapa nchini ambaye hakuona mchango wa Hamisi Tambwe, na kama hatutobadilika kama wenzetu basi tutachekwa kila siku na tutarusha ngumi kila siku kwani wenzetu hatuwaoni walivyojawa na furaha sasa na wakitutania sisi tuleta lugha za matusi na ugomvi badala ya kubadilika na kuuchukulia utani wetu kama changamoto ya kutumbusha jambo, Yanga oyeeee, ila pia hongereni watani zangu kwa madiliko yenu na ndiomana muna furaha sasa, munafurahia mulichokitengeneza

    ReplyDelete
  4. Madeni fc! Tambwe kaza baba,, hd wakulipe! Jasho lako lisiende bure

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic