February 14, 2021


 
BEKI mkongwe ndani ya kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes amesema kuwa wana nafasi ya kufanya vizuri kwenye hatua za kimataifa kutokana na wachezaji kuwa na morali wa kusaka ushindi ndani ya uwanja.

 Simba ipo kundi A hatua ya makundi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, ipo kundi moja na Al Ahly ya Misri,Al Merrik ya Sudan na AS Vita ya Congo.

 Mchezo wake wa kwanza kimataifa ilishinda bao 1-0 dhidi ya AS Vita, Februari 13, nchini Congo ina kibarua cha kuvaana na Al Ahly ya Misri Februari 13, Uwanja wa Mkapa.

 Akizungumza na Spoti Xtra, Kapombe alisema kuwa kila siku wamekuwa wakikumbushana kuhusu malengo yao kimataifa jambo ambalo linawapa nguvu ya kuzidi kupambana.

“Kila wakati tunapokuwa pamoja kambini, mazoezini tunakumbushana kuhusu malengo ya timu hivyo jambo hilo linatupa nguvu ya kufanya vizuri kimataifa, mashabiki watupe sapoti tuna amini tutafikia malengo yetu,” alisema.

 Kapombe ni chaguo la kwanza la Gomes pia hata zama za Sven Vandenbroeck ambaye kwa sasa yupo na Klabu ya FAR Rabat alikuwa chaguo la kwanza na alicheza mechi zote za kimataifa ikiwa ni pamoja na ile ya Plateau United ya Nigeria na FC Platinum ya Zambia.

2 COMMENTS:

  1. Sahihisha hapo juu, sio tarehe 13 mchezo wa Simba na Al Ahli, bali 23 February

    ReplyDelete
  2. Gongowazi wayasikie maneno ya wenye akili ya kujenga sio ya kubomoa. Nawasihi nao wabadili nio zao huenda wakaongoka. Mimi nawapenda sana Simba kutokana na suluki na jinsi wanavoheshimiana na wala huwasikii kutukana. kuzomea au ubishi pale wanaposhindwa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic