February 22, 2021


 MSHAMBULIAJI wa zamani wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe amefunguka kuwa Yanga bado hawajamlipa fedha zake anazodai Sh milioni 42 licha ya siku 45 walizopewa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kumalizika.

 Tambwe ametoa kauli hiyo baada ya siku 45 zilizotolewa na Fifa kumalizika bila kuwepo kwa dalili za malipo hayo.

 

Tambwe amesema mpaka sasa hajua chochote juu ya malipo ya fedha zake kutoka Yanga licha ya kuwapa hesabu zote kwani hata wakili wake, Felix Majani hajui lolote kutoka ndani ya timu hiyo licha ya siku walizopewa kumalizika.

 

“Binafsi hakuna ambacho kwa sasa najua kutoka Yanga zaidi ya kwamba bado hawajanilipa licha ya kupigiwa simu na Injinia, Hersi Saidi na kuniambia nifanye mahesabu ya pesa ambazo nawadai, mwanasheria wangu amefanya hivyo, akawatumia lakini hakuna jambo lolote jipya.

 

"Ninachojua kwamba Fifa waliwapa siku 45 wawe wameshalipa lakini hadi sasa zimeisha na hakuna lolote, hivyo hawezi kufanya usajili wowote katika usajili ujao hadi wawe wamelipa na kuwasiliana na mwanasheria wangu ili arudishe taarifa Fifa,” amesema Tambwe.


Chanzo:Championi

16 COMMENTS:

  1. Vipi timu kubwa kama ya Yanga ambayo wameweza kutumia kutumia mabilioni kuijenga timu hiyo, washindwe leo kumlipa Tambwe kumlipa milioni arbaini. Si bure hapo pana kitu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ndio faida ya kuwa na viongozi kama akina Mwakalibela yanga wanavuna walichokipanda.

      Delete
  2. Sasa hizi ni kero kila siku Tambwe Tambwe Tambwe anadai anadai zinaboha hizi habari

    ReplyDelete
  3. Zina boha haki ya mtu.Pitisheni michango ksma zinawakera.
    Ni dharau mtu anadai hski yake yake na kuliko upaze sauti alipwe eti "inakuboha".
    Ingekuwa ni jasho lako usinge comment huu utumbo.

    ReplyDelete
  4. Unajua Yanga inawachanganya bt mzee na blog yako tunakutakia uendelee kuishi na u friends of Simba(Wazee wa football fitna.Sasa tutaendelea kutoa maoni Lin habari nyingine ni vichekesho.Hukumu ilitoka na masharti yake bt why u unataka uweke deadline zako.Bt Carinhos yupo sanaaaaa

    ReplyDelete
  5. Sasa sisi tufanyeje aendelee tu kudai hamna namna😊

    ReplyDelete
  6. Hapa Yanga sasa wanatakata kutoa boko mchana kweupe

    ReplyDelete
  7. Inaonesha hawajali ile adhabu ya kupigwa marufuku ya kutosajili wachezaji wapya kwa muda wa miaka mitatu ambao wachezaji wa sasa wote watakuwa wameshamaliza muda wao na kusepa.

    ReplyDelete
  8. Tambwe hawadai Yanga.Hii ni njama ya FIFA ili Simba achukue ubingwa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hakika wewe ni punguani kweli kweli. Ulichoongea ni utumbo kabisa. Inaelekea Utopolo mnamuogopa Sana Simba maana si kwa uchangiaji huo

      Delete
  9. Ohoo, sasa wanaanza kuivaa hata FIFA. Lazima mufahamu FIFA sio chombo cha kukitania au kukichezea, hichi ni chombo kikubwa kinachoheshiimiwa kode duniani kama hujui

    ReplyDelete
  10. Sio jipya kwa uto dante yondani picha ni zilezile za tambwe

    ReplyDelete
  11. Kumlipa tambwe mpaka tuchukue ubingwa VPL kama inawauma mlipeni nyinyi ili muenderee kusajili cc wanainhi tuko vzuri mpaka 2021/2029/ tibazongizaaaaa

    ReplyDelete
  12. Daaah, hii sasa ni atar sanaah, Ila jamaa alipwe stahiki zake tusijejipatia matatizo ya kushuka daraja buree

    ReplyDelete
  13. Halipwi mtu hapa mpaka turejeshewe Morrison. kwanza raisi wa FIFA ni rafiki wa Mo naona njama ya kuihujumu yanga imehamia FIFA.

    ReplyDelete
  14. Utopolo walipe pesa waache ujanjaujanja lungu zito litawashukia FIFA sio TFF msije mkatia huruma huko mbele ya safari

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic