February 13, 2021

 


CEDRIC Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa anaamini wachezaji wake wote ndani ya kikosi wana kazi ya kucheza kwa ushirikiano jambo litakalompa matokeo chanya ndani ya uwanja kuelekea kwenye mchezo dhidi ya Mbeya City.

Kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya African Sports uliochezwa wikiendi aliweza kutengeneza pacha mbili ambazo zilianza kujibu taratibu jambo ambalo anaamini litamfanya kuwa bora ndani ya uwanja.


Pacha hiyo ni ile ya Haruna Niyonzima  ambaye aliweza kucheza kwa maelewano na ingizo jipya lililotumia dakika 10 bila kugusa mpira ndani ya Uwanja wa Azam Complex, Fiston Abdoul Razack pamoja na ile ya Tuisila Kisinda dhidi ya Muangola, Carlos Carinhos.


Akizungumza na Saleh Jembe, Kaze amesema kuwa amewaona wachezaji wake namna ambavyo wanacheza ndani ya uwanja jambo ambalo linampa matumaini ya kufanya vizuri.


“Naona wachezaji wanapambana ndani ya uwanja, pia uwepo wa mchezaji wetu mpya Fiston taratibu unazidi kuleta nguvu ndani ya kikosi jambo ambalo linatufanya tupate kile ambacho tunakihitaji.


“Kwenye mchezo wetu dhidi ya Mbeya City tupo tayari na tunatambua kwamba utakuwa mchezo mgumu nasi tutapambana ili kupata pointi tatu,” amesema.

Yanga ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 44 ikiwa imecheza mechi 18, leo Februari 13 inakutana na Mbeya City iliyo nafasi ya 18 na ina pointi 14.

 

5 COMMENTS:

  1. AS VITA 0 SIMBA 1
    Yako wapi matamanio ya gongowazi AKA utopolo..Ndiyo tena tusikie kelele za wale Eyimael aliita mbumbumbu kazi kupiga kelele utadhani mbwa na nyani ...baaa baaaa baaa
    matano matano nadoo ndiyo ulikuwa wimbo. tafuteni mwingine..mtakereka sana

    ReplyDelete
  2. Haihitajii yote hayo, Mbeya siyo kama As Vita, katika taratibu Mbeya ni ya mwisho kabisa, msicharuke na mkajigamba kama vile mnakwenda kucheza na mabingwa. Wacheni majigambo yasiyo na mana kwani Yanga ni timu kubwa

    ReplyDelete
  3. Magongowazi wakiomba na kutaraji Mnyama atapigwa tano ziro kama hali ilivo katika zama za Uchebe lakini juu ya hivo wakafikia robo fainali. Mungu ni Mkubwa tazama alivofungua njia na siku njema huanzia asubuhi na tunachohitaji sasa ni droo bas. Mnyama anajitayarisha kupambana na Mabingwa wa jadi wa Africa na huku matopolo wakijitaysrisha kupambana na Mbeya City Hahahaaa Raha tupu

    ReplyDelete
  4. Saleh jembe acha kuandika habari ukachanganya na dhihaka.eti alicheza dakika kumi bila kugusa mpira..hiyo inaendana vipi na content?

    ReplyDelete
  5. Kwani kwa lambalamba ilikuwaje?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic