March 13, 2021


 


BEKI wa kulia wa AS Vita, Shabani Djuma amekiri kuwa ni kweli alifuatwa na viongozi wa Simba ili kuangalia uwezekano wa kujiunga nao mwishoni mwa msimu.

Djuma amekuwa katika kiwango bora ndani ya AS Vita ambapo msimu huu katika michuano yote aliyoichezea timu hiyo amefunga mabao 6 na kutoa pasi tano za mabao.

Akizungumzia uwezekano wa kutua Simba Djuma amesema: “Ni kweli kuna baadhi ya viongozi wa Simba walinitafuta kwa ajili ya mzungumzo ya awali ya usajili lakini siwezi kulizungumzia sana hilo kwani sasa.

"Hii ni kwa sababu wote kwa sasa tunapambana kuzisaidia timu zetu zifanye vizuri katika michuano ya kimataifam ikizingatiwa tupo kundi moja.

Kutokana na uwezo wa beki huyo, ni wazi endapo beki atafanikiwa kujiunga na Simba ataenda kugombea namba na Shomari Kapombe ambapo utakuwa mtihani mgumu kwa kocha kuchagua nani wa kuanza kulingana na ubora wa mabeki hawa.

 

 

 

 

 

5 COMMENTS:

  1. Mimi naona tatizo kubwa la simba kwa sasa ni mshambuluaji sio beki namba 2

    ReplyDelete
  2. Ushambuliaji hakuna tatizo na ndio mana inaongoza kwa wingi wa msgoli

    ReplyDelete
  3. Djuma Kama Simba wapo serious basi ni investment nzuri ila kila siku zikienda mbele kwenye mashindano ya caf klabu bingwa ndipo vilabu vyengine venye nguvu zaidi ya pesa vinavyomuona na itakuwa ngumu kwa Simba kuja kushindana na kumtwaa.

    ReplyDelete
  4. Kama anafanya vzr A.Vita ni Bora aendeleee kubaki lkn anaweza kujuta kea kuja na kukalia banchi awehana tofauti na mchezaji wa Kikosi cha B, kuonekana akiwa Congo ni rahisi kuliko akiwa Simba, Vita umeingia marangapi hatua ya Robo kama ni mchezaji mzuri ataonekana tu.
    Asome majira ya wakati vinginevyo atajuta

    ReplyDelete
  5. Kwani beki line ya simba imeruhusu magoli mangapi?aje tu ila simba haina shida ya beki bali inatakiwa kuongea mshambuliaji mwenye makali zaidi ya Akina kagere na mugalu na boko. Lwanga,kapombe, wawa,joash, duchu wanatakiwa wapewe muda tu mbona wako sawa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic