KIKOSI cha Taifa Stars kimeanza safari ya kuelekea nchini kwa
ajili ya michezo miwili ya kujipima nguvu dhidi ya kikosi cha timu ya Taifa ya
Kenya.
Stars inataka kuitumia michezo hiyo hiyo ambayo inatarajiwa kupigwa Machi 15, na 18 mwaka
huu kama sehenu ya maandalizi ya michezo ya kusaka tiketi ya michezo ya kufuzu
fainali za kombe la mataifa ya Afrika (AFCON), dhidi ya Equatorial Guinea na
Libya.
Stars chini ya kocha, Kim Poulsen ilianza kambi rasmi siku ya Jumatatu iliyopita katika uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
Akizungumzia maandalizi yao mchezaji Mwandamizi, Juma Kaseja amesema: “Kikosi kimekuwa na wasaa mzuri wa mazoezi ya kujiandaa na michezo yetu dhidi ya Kenya na ile ya kutafuta tiketi ya kufuzu AFCON.
"Tunajua mbele ya Kenya haitakuwa michezo rahisi kutokana na ukweli kwamba tunajuana vizuri, lakini kutokana na ari niliyoiona kwa wachezaji naamini tutafanya kitu kizuri,"
0 COMMENTS:
Post a Comment