March 6, 2021


ZILE fitina ambazo Simba walifanyiwa kwenye mchezo wao wa hatua ya awali dhidi ya Plateau United ya Nigeria kwa kutaka kuwatengenezea Corona feki baadhi ya wachezaji nyota zimekwama kwa Wasudan.

Miongoni mwa wachezaji ambao walikuwa wanatajwa kutengenezewa Corona ilikuwa ni Luis Miquissone pamoja na Clatous Chama jambo ambalo lilileta hofu kwa muda ila mwisho wa siku nyota hao walicheza kwenye mchezo huo na ubao ulisoma Plateau United 0-1 Simba.

Leo, kikosi cha Simba ambacho kipo nchini Sudan kimekamilisha masuala ya vipimo vya Corona na majibu kutolewa kwamba hakuna nyota wa timu hiyo mwenye maambukizi ya Corona.

Hivyo miongoni mwa nyota ambao wanaweza kuonyesha makeke yao uwanjani ni pamoja na mchezaji aliyewafunga Al Ahly na bao lake kuwa bora ndani ya wiki kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Luis Miquissone.

Mchezo wa leo wa kundi A unatarajiwa kuchezwa majira ya saa 10:00 jioni na unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili.

Habari zinaeleza kuwa kwa sasa wachezaji wote wa Simba wapo kwenye uangalizi mkubwa ili waweze kuwa salama pamoja na mipango makini inayofanywa na viongozi wa timu hiyo wakiongozwa na Mtendaji Mkuu, Barbara Gonzalez.

Mratibu wa Simba, Abbas Suleman amesema kuwa kila kitu kipo sawa na wachezaji wana morali ya kusaka ushindi kwenye mchezo wa leo.

Leo saa 10:00 kikosi cha Simba kitakuwa na kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Al Merrikh ya Sudan ambayo bado haijakusanya pointi na inahitaji kushinda leo mbele ya Simba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic