OLE Gunnar Solskjaer, Kocha Mkuu wa Manchester United amekiri kuwa anapata hofu kuhusu kushuka kwa kiwango cha timu yake na kushindwa kufunga mabao baada ya sare ya 0-0 dhidi ya Crystal Palace, Jumatano ugenini, ambayo imewafanya wawe nyuma ya vinara, Man City kwa tofauti ya pointi 14.
Manchester United sasa imecheza mechi tatu mfululizo bila kupata bao, mbili zikiwa ni za Premier na moja ya Ligi ya Europa.
Kocha huyo wa Man United, amesema: “Wakati mwingine haufikii kile kiwango ulichonacho na ulichokuwa nacho kwa miezi mingi sana.
" Inaleta hofu bila shaka lakini najua kwamba vijana wanajitoa kwa kila kitu.
"Tunacheza kila baada ya siku tatu na najua wanajitoa kwa kila kitu walichonacho. Ninafurahishwa na hilo. Dean Henderson alidaka badala ya David de Gea ambaye alitajwa hakuwepo kutokana na sababu binafsi, na Dean hakuruhusu bao huku akiiokoa United kufungwa bao dakika ya mwisho.
Alipoulizwa kama De Gea atakosekana katika dabi ya Jumapili dhidi ya Manchester City, Solskjaer aliongeza: “Siwezi kuzungumza kuhusu David. Ni suala binafsi. Dean yupo tayari kama akihitajika.”
0 COMMENTS:
Post a Comment