March 12, 2021


KOCHA mkuu wa Simba, Didier Gomes, amesema kuwa, matokeo ya mchezo wao uliopita dhidi ya Tanzania Prisons, yamewaongezea kitu katika hesabu zao za kuwamaliza Al Merrikh ya Sudani, ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba na Al Merrikh wanatarajia kucheza mchezo wao wa marudiano wa kundi A Jumanne ijayo, mchezo utakaopigwa kwenye uwanja wa Mkapa Dar es Salaam, huku wakiwa na kumbukumbu ya suluhu kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa Machi 6.

Juzi Jumatano, Simba walilazimika kusubiria mpaka dakika ya mwisho ya mchezo kuweza kusawazisha bao la kuongoza la Prisons, katika mchezo wa sare ya bao 1-1 uliopigwa kwenye uwanja wa Mkapa.

Akizungumzia mipango yao kuelekea mchezo dhidi ya Al Merrikh Gomes amesema: “Hatukufurahishwa na matokeo ya mchezo wetu uliopita dhidi ya Prisons, lakini tumechukua hiyo kama changamoto hivyo tumejipanga kuhakikisha tunarejea tukiwa bora kwenye mchezo ujao dhidi ya Al Merrikh.

“Naamini vijana wangu watakuwa na  wakati mzuri dhidi ya Al Merrikh, na ni lazima tucheze katika levo ambayo tulicheza dhidi ya Al Ahly na As Vita,”

 

5 COMMENTS:

  1. Goal lenyewe offside daaa kumbe simba walkuwa 13 na ranziman

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hivi lazima ucomment kila habari! Na goli lililokataliwa unaliongeleaje?

      Delete
    2. Achana na utopolo ana stress wao goli lao na polisi mbona hawazungumzii

      Delete
    3. Kwa kweli nawaonea huruma Simba hasa baada ya kunyimwa penalt ya wazi kabisa baada ya kapombe kuangushwa ndani ya kumi na nane.Picha za marejeo za kipenga Cha mwisho zikionesha wazi beki wa prison akiukamata mkono wa kapombe na kumuangusha chini. Isitoshe Simba walinyimwa goli halali kabisa ambalo Kama lingekubaliwa basi simba wangekuwa na uwezo wa kupata magoli mengi zaidi kwani takwimu zinasema timu kubwa Duniani wakikufunga mapema uwezekano wa kuongeza magoli mengi zaidi ni mkubwa mno.Marefa wetu bado kabisa na hawapo fiti kuendana na Kasi ya mchezo.Labda kwanini kusitumike waamuzi sita kusimamia mechi.Marefa wawili wawe kazi yao ni kuangalia matukio ya kwenye goli na penalt box tu.

      Delete
  2. Prison msimu wanabebwa na marefa mechi za Simba dah! Shinyanga walibebwa, kwamkapa wamebebwa lakini wanaume hatushikiki na Wala hatutishwi kombe letu tu kila mmoja anajua

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic