March 12, 2021

 


KOCHA msaidizi wa klabu ya AS Vita ya nchini Congo, Raoul Shungu amesema kuwa yupo tayari kuisikiliza ofa ya Yanga kama watahitaji aje kuifundisha timu hiyo.

Yanga tayri imemtambulisha kocha Juma Mwambusi kama kocha wa muda  wa timu hiyo, huku mchakato wa kumsaka mbadala wa Kaze aliyefutwa kazi Jumapili iliyopita ukiendelea.

Shungu mwenye uraia wa Congo DR, aliwahi kuwa kocha mkuu wa Yanga na kuipa ubingwa wa Ligi Kuu msimu wa mwaka 1998/99 na kuondoka mwaka 2001 na nafasi yake ilichukuliwa na kocha Boniface Mkwasa.

Akizungumzia mpango huo Shungu amesema: “Nimesikia kuwa aliyekuwa kocha mkuu kwa sasa hayupo, sijawasiliana na kiongozi yeyote wa Yanga juu ya kuwa kocha wao lakini kama watakuwa wananihitaji basi nitasikiliza ofa yao ipoje kwangu.

“Nishawahi kuwa kocha wa Yanga, mpira wa Tanzania naufahamu vizuri na changamoto zake nafurahi niliishi vizuri wakati nipo Tanzania, muda mwingine napaona kama nyumbani,”


4 COMMENTS:

  1. utopolo wanachekesha! kocha msaidizi wa DR Congo Zahera aliwashinda itakuwa huyo msaidizi wa AS Vita

    ReplyDelete
    Replies
    1. Siyo kazi yako,na haikuhusu umbeya wa kiume huo,utelembwe vp?

      Delete
  2. povu la nini utopolo...wakati habari yenyewe ni feki...kama Zahera alisema Simba hawana hela ya kumplipa Ibenge...Sasa Yanga ndiyo wana hela ya kumlipa msaidizi wa Ibenge?wasijetembeza bakuri

    ReplyDelete
  3. Kocha wa Barcelona kachemka pale utopolo sembuse As vital .
    Team ishaoza Sasa inatoa harufu tu, ikioza imeoza tu team

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic