UONGOZI wa Klabu ya Al Merrikh ya Sudan umethibitisha kumfuta kazi Nasreddine Nabi na wasaidizi wake Hamad Sagheer na El Dao Gadamelkhair kutokana na matokeo mabovu katika mechi za kimataifa.
Timu hiyo inashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa hatua ya makundi na ipo kundi A pamoja na Klabu ya Simba ambapo mwendo wake ulikuwa ni kusuasua.
Nafasi yao kwa sasa ipo mikononi mwa Lee Clark ambaye anakuwa mrithi wa mikoba ya Nass ambaye mchezo wake wa mwisho ilikuwa dhidi ya Simba ya Tanzania.
Kwenye mchezo huo uliochezwa jana, Machi 6, Uwanja wa Al Hilal ubao ulisoma Al Merrikh 0-0 Simba jambo ambalo limewafanya mabosi wa timu hiyo kumchimbisha.
Kwenye mechi mbili za kimataifa za nyuma alipoteza zote na kuyeyusha pointi sita hivyo kwa sasa timu hiyo ina pointi moja ikiwa inaburuza mkia.
Licha ya kwamba inaburuza mkia bado kundi lipo wazi ikiwa itachanga karata zake vema na kupata ushindi kwani kinara Simba ana pointi 7 huku timu mbili ambazo ni AS Vita na Al Ahly zote zina pointi nne kibindoni.
Ongeza nyama kidogo, huyo Lee Clark ni nani na anatokea wapi hadi kupatika ktk kipindi kifupi tuu cha chini ya saa 12. Au walikuwa wamemuandaa wakitegemea hilo lililotokea?
ReplyDeleteToa wasifu basi duuu waandishi wetu bn,,,
ReplyDelete