UKUTA wa
Klabu ya Yanga unaoundwa na nahodha Lamine Moro raia wa Ghana na mzawa Bakari
Mwamnyeto ambaye ni msaidizi unapata tabu kwa kuokota mabao mengi nyavuni
tofauti na ule wa watani zao wa jadi Simba unaoongozwa na Joash Onyango na
Pascal Wawa.
Kwenye mechi
tano za hivi karibuni ambazo Yanga imecheza imeruhusu jumla ya mabao 7 na
kwenye harakati za kusaka pointi 15 iliambulia pointi 6 na kuyeyusha pointi 9
huku ule wa Simba ukiruhusu mabao matatu.
Mwendo wao
ulikuwa namna hii:-Tanzania Prisons 1- 1 Yanga, Mbeya City 1-1 Yanga, Yanga 3-3
Kagera Sugar, Yanga 1-0 Mtibwa Sugar, Coastal Union 2-1 Yanga.
Watani zao
wa jadi chini ya Wawa na Onyango kwenye mechi zao tano za hivi karibuni ndani
ya ligi wameokota jumla ya mabao matatu nyavuni.
Mbali na kuokota nyavuni mabao hayo matatu pia
walipokuwa wakisaka jumla ya pointi 15
kwenye mechi hizo za ligi, waliweza kusepa na jumla ya pointi 13 na kuyeyeyusha
pointi mbili kwa kuwa walilazimisha sare mbele ya Azam FC.
Mwendo wao
ulikuwa namna hii:- Simba 4-0 Ihefu, Dodoma Jiji 1-2 Simba, Simba 2-2 Azam FC,
Biashara United 0-1 Simba, Simba 3-0 JKT Tanzania.
Cedric Kaze,
Kocha Mkuu wa Yanga ameliambia Spoti Xtra kuwa katika hilo hana wa kumlaumu
zaidi ya kufanyia kazi makosa ambayo wameyafanya.
Didier
Gomes, Kocha Mkuu wa Simba ameliambia Spoti Xtra kuwa amekuwa akiwaambia
wachezaji wao jukumu lao ni kutafuta ushindi ndani ya uwanja.
Nakumbuka huko nyuma kulikuwa na habari kuwa lamine ampoteza wawa, sasa hadithi imebadilika
ReplyDeleteNa huyo Mwamnyetu alisajiliwa kwa mbwembwe kubwa sana aliteremka Dar Salam kwakuwa anakuja kujiunga na Mnyama lakini alipofika matopolo wakamteka wao na kusajili kwa kejeli na kila aina ya mbwembwe na huku wakitishia pia kumngowa Chama na Senzo na wachezaji wengine. Kumbe zilikuwa mbio za sakafuni na mwanzo na kuishi ukingoni
ReplyDeleteAcha kuamini baadhi ya habari za kwenye magazeti sometimes vichwa vya habari na habari zenyewe hutungwa ili magazeti yanunuliwe
DeleteSimba waligomea dau alilotaka mwamnyeto wakasema haliendani na uwezo wake, alivyokuja dar alikuja kwa ajili ya yanga na wala sio simba
Delete