March 15, 2021

 


BAADA ya uongozi wa Simba kupitia kwa Mtendaji Mkuu, Barbara Gonzalez kuandika barua kwa Shirikisho la Soka Afrika, (Caf) kuomba ufafanuzi juu ya wachezaji wawili wa Al Merrikh waliocheza mchezo dhidi yao wakiwa wamefungiwa imeelezwa kuwa majibu yametolewa kwamba wachezaji hao hawana makosa.

Wachezaji hao wawili ambao ni Ramadhan Agab na Bakhit Khamis walicheza Machi 6, Uwanja wa Al Hilal kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, hatua ya makundi na ulikamilika kwa sare ya bila kufungana.

Habari zillieleza kuwa wachezaji hao wawili walikuwa wamefungiwa kucheza kwa kuwa kulikuwa na makosa kwenye mikataba yao  jambo ambalo liliwafanya Simba kuhitaji ufafanuzi kutoka Caf.

Endapo ingebainika kwamba wachezaji hao walicheza kwa makosa kwenye mchezo huo basi Simba ingepewa pointi tatu za mezani na kuifanya ifikishe pointi 9 kwa kuwa ilikuwa ina pointi sita kabla ya kucheza nao na wakati huu ina pointi 7.

Taarifa zimeeleza kuwa Caf wamewaambia Simba kwamba wachezaji hao walikuwa wamefungiwa kucheza ligi ya Sudan lakini wanaweza kucheza mashindano yanayosimamiwa na Caf.

Hivyo kwa taarifa hiyo ni kwamba kesho wachezaji hao watakuwa sehemu ya kikosi kitakachomenyana na Simba, Uwanja wa Mkapa kusaka pointi tatu na Simba haitapata pointi tatu.

Al Merrikh ikiwa kundi A inaonekana inaweza kuwa kikwazo kwa Simba kesho kwa kuwa ina pointi moja na kundi lipo wazi ikiwa itashinda kesho itafufua matumaini ya kufuzu robo fainali.

Pia ilifanya mabadiliko kwenye benchi la ufundi jambo linalowafanya waje na mbinu mpya kusaka ushindi hivyo lazima Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes kujipanga kusaka pointi tatu.

11 COMMENTS:

  1. Vita ni vita tuu, el merreck wapigwe

    ReplyDelete
  2. Sasa mbona Rage Alisema Simba itapewa points ikithibitika walikua na mikataba mibovu, naanza kupata wasiwasi na Rage kunakipindi anaongea kuwafurahisha watu lkn Hana uhakika na anachosema,
    Nakumbuka pia aliwahikusema Suala la Kichuya Simba lazima ilipe lkn kumbe hata tukio lenyewe hakijui...

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ndugu yanga inaelekea humjui vizuri huyu jamaa!!!!!Ni bonge la mbabaishaji anaejua vizuri kucheza na saikolojia za watu,jaribu kufuatilia enzi zake alipokuwa anagombea na hatimaye kuwa katibu mkuu wa DRFA kisha alipokuwa katibu mkuu wa TFF na hata wakati alipokuwa Simba pambio zake zote zilikuwa zinafanana

      Delete
  3. Msiwe na wasiwasi paka wetu wameruhusiwa na CAF kuingia uwanjani

    ReplyDelete
  4. pambaneni watani ulaya vitu hivi hakuna

    ReplyDelete
    Replies
    1. SIMBA HAWAKUOMBA POINT 3 TUREJEE HATA BARUA YA BARABARA GONZALEZ KWENDA CAF. MORRISON KAWAZIDI AKILI VIPI MTAWEZANA NA SIMBA

      Delete
  5. Na kwa hakika kesho simba hamtaamini kitakachotokea. Mark this post. Safari ya kufuzu bado sana...

    ReplyDelete
    Replies
    1. dua zako za kuku! kama hawakuamini Kinshasa na pale Al Ahly walipokuja Dar ndiyo itakuwa kesho...jiongeze acha kutesa moyo wako na matumaini ya roho maskini

      Delete
  6. Rage ni wa mwaka 47 alishapitwa na wakati..tehtehteh

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic